USIPITWE NA KINACHOJIRI SASA KWENYE KILIMO CHA MAHINDI NA JATU KITETO, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Tunaendelea kuwajulisha wanachama wote ambao wameshiriki katika mradi wa kilimo cha mahindi na JATU ambacho kinalimwa Kiteto – Manyara kuwa kwa sasa zao hilo liko katika hatua nzuri sana na tayari mazao yetu mengi yameanza kutoa mahindi.

Hata hivyo kulingana na hali ya hewa inayoendelea kwa sasa ya mvua lakini inaonekana zao la mahidi likiwa imara na likizidi kuimalika zaidi siku hadi siku.

Hadi kufikia hatua hii bado hatujapata hasara yoyote kulingana na hizi mvua zinazoendelea kunyesha na hatutarajii kupata hasara kwani bado tunaendelea kujipanga kwa kuzingatia ushauri kutoka kwa watafiti pamoja na wataalamu wa kilimo ambao wako ndani ya kampuni.

Aidha kwa wakulima wanaolima na Jatu zao hili la mahindi wanatakiwa kutegemea mavuno mengi zaidi ya msimu uliopita kutokana na matokeo yaliyopo pamoja na hali ya mazao yanavyo onekana kwa sasa ni nzuri sana.

Tunatarajia kufikia mwezi wa sita mwaka huu zoezi la mavuno litaanza ambapo kwa kila ekari moja tunatarajia kupata gunia zisizo pungua 30.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s