JATU SUPER DINNER YAONGEZA KIU YA MAFANIKIO KWA WADAU WA KILIMO NCHINI, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Baada ya ile hafla iliokua ikisubiriwa kwa hamu kwa miezi kadhaa yaani usiku wa JATU Super Dinner kukamilika jumamosi ya tarehe 14/03/2020 huku ikiwa na kaulimbiu ya uwekezaji kwenye kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji Kiteto, Manyara. Wadau wa kilimo nchini wameupokea mradi wa uwekezaji kwenye kilimo cha kisasa kwa mikono miwili, ilikua ni ndoto ya watanzania wengi kushiriki kwenye kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji ila kutokana na changamoto mbalimbali imekua ngumu wengi kufanikiwa, kwasasa kutokana na ambavyo JATU imejipanga kutekeleza mradi huu mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji unaofanyika wilayani Kiteto umerudisha imani na kiu ya wadau wa kilimo kuwekeza kwenye kilimo.

Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikua Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stella Manyanya imefanikiwa kwa asilimia kubwa kuleta ushawishi kwa wadau mbalimbali ambao hapo mwanzo walikata tamaa ya kuwekeza kwenye kilimo. Akiongea kwenye hafla hiyo Mh. Manyanya amewataka wadau wa kilimo kushirikiana na JATU kuboresha sekta ya kilimo nchini kwa kuwekeza kwa pamoja kwenye miundombinu na vifaa vya kisasa kwenye mashamba ili kuongeza tija kwa wakulima na pia kuongeza mtaji kwenye SACCOS ya JATU ili kuweza kutoa mikopo mingi zaidi kwa wakulima hasa kwa vijana na vikundi vya kinamama.

Hata hivyo wadau mbalimbali waliohudhuria wameonesha kuridhishwa na mpango mkakati wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Kiteto na kuwataka viongozi wa JATU kuwa makini kwenye kuzitumia rasilimali zinazotolewa na wadau ili ziweze kutumika kama ilivyopangwa na hatimae kutimiza malengo ya kiuchumi kwa washiriki wote wa miradi hiyo. Mkurugenzi wa JATU Ndg. Peter Isare ameahidi kuwa JATU itaendelea kuandaa hafla zingine za kukutanisha wadau wa uwekezaji ili kuweza kuunganisha nguvu na kufanya uwekezaji wa pamoja kwa manufaa ya watanzania wote. Pia amewataka vijana kujiamini na kutokatishwa tamaa na mawazo yao mazuri yaliolenga kuboresha sekta ya kilimo nchini bali wayalete JATU ili tuweze kuyaboresha na kuhakikisha yanasaidia jamii kuondokana na umasikini.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s