NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MH. ENG. STELLA MANYANYA AHIMIZA WADAU KUSHIRIKIANA NA JATU KUONGEZA TIJA KWENYE SEKTA YA KILIMO NCHINI, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Stella Manyanya  amewataka wadau wa kilimo nchini kushirikiana na JATU kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa cha umwagiliaji ili kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo nchini pia ameiomba kampuni ya JATU PLC kuendelea na uaminifu kwa wanachama wake katika kutoa mikopo nafuu isiyokuwa na riba kwa wakulima pamoja na kulinda mali za wanaowekeza katika kampuni hiyo.

Mh. Manyanya aliyasema hayo siku ya jumamosi katika usiku wa hafla ya ‘Jatu Super dinner’ ambapo JATU iliwaalika wageni mbalimbali kuja kuzielewa fursa za uwekezaji kwenye kilimo na namna JATU ilivyojipanga kuboresha maisha kwa wakulima.

“Hiki  ndicho kilio chetu  katika kubuni mambo mazuri, vijana wanamawazo mazuri kinachotakiwa kuwasukuma kidogo tu, hivyo nawaomba JATU muendelee kuwapa imani wanachama wenu kama mnavyoendelea hivi sasa” alisema Waziri Manyanya.

Pia Manyanya ameiomba serikali kukubali mawazo mapya ili kufikia malengo wanayoyahitaji na ameahidi ushirikiano wa hali na mali kwa kampuni ya JATU.

Mkurugenzi Mtendaji wa JATU, Peter Isare amesema kuwa  kampuni hiyo imedhamiria kutokomeza umasikini kupitia rasilimali watu, kilimo, viwanda, mikopo na masoko. Katika hafla hiyo ambayo ilifana kwa namna yake na wageni wengi kupata elimu juu ya uwekezaji kwenye kilimo cha kisasa, Isare alizungumzia mambo mawili makuu ambayo ni dhima na dira ya JATU ambayo imejikita kwenye kujenga afya na kutokomeza umasikini. Baada ya kufanya uchunguzi wa kina na kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima na watanzania kiujumla alisema kuwa JATU imejipanga kuondoa umasikini huku akiwataka waliokuwa na mitaji ila hawana muda kushirikiana na JATU kuwekeza kwani wanaowataalamu wakutosha wanaosimamia miradi kwa kusimamia misingi bora ya kilimo cha kisasa ili kuhakikisha wawekezaji wanapata mavuno yenye tija huku kampuni ikiwahakikishia soko kupitia kwenye viwanda vyake.

Wakati huo huo Isare amesema kuwa JATU wanaendelea kuboresha miradi yao mbalimbali ikiwemo ile ya kilimo ili kuzidi kuleta tija zaidi kwa wanachama wao.

“JATU inatambua namna miradi ya kilimo inavyohitaji rasilimali fedha ili kulifanya zoezi hilo kuwa rafiki kwa wanachama wake hivyo kampuni iliamua kuanzisha saccos yake (JATU SACOSS LIMITED), ambayo ilisajiliwa rasmi kwa lengo la kuwakopesha wakulima wake mikopo nafuu na isiyo na riba, lakini pia sacoss hiyo hutoa mikopo midogo midogo ya kimaendeleo yenye masharti nafuu” alisema Isare.

Dhamira yetu kubwa ni ifikapo mwaka 2022 kuona watu wanatambua rasilimali walizonazo na namna ya kuzitumia ipasavyo hivyo kupitia programu yao mpya ambayo amezinduliwa siku hiyo ya ‘JATU Talk’ ambayo itapatikana katika simu ya kiganjani ‘Play/App store’ itawawezesha vijana kutoa mawazo mbalimbali yatayolenga kuboresha maisha ya watanzania kupitia sekta ya kilimo, viwanda, mikopo na masoko.

Aidha amemalizia kwa kusema kuwa JATU inategemea kuingiza sokoni sehemu ya hisa zake ili kuwawezesha kutekeleza mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji unaopatikana Kiteto mkoani Manyara anaogharimu kiasi cha bilioni 7.5 fedha za kitanzania.

Aidha Meneja Mkuu wa JATU, Issa Simbano aliongeza kuwa miradi ya JATU inawajumuisha watanzania wote bila kujali eneo alilopo. Alisema kuwa mpaka sasa JATU na wanachama wake wamefanikiwa kuwekeza kwenye zaidi ya ekari 15,000 nchi nzima ikijumuisha mradi wa kilimo cha mpunga unaofanyika mkoani Morogoro wilaya ya kilombero wenye takribani ekari 5,000, kilimo cha mahindi na alizeti unaofanyika mkoani Manyara wilaya ya Kiteto wenye takribani ekari 10,000, kilimo cha maharage na machungwa unaofanyika mkoani Tanga wilaya ya kilindi(maharage) wenye takribani ekari 3000 na wilaya ya handeni na muheza wenye takribani ekari 1000.

2 thoughts on “NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MH. ENG. STELLA MANYANYA AHIMIZA WADAU KUSHIRIKIANA NA JATU KUONGEZA TIJA KWENYE SEKTA YA KILIMO NCHINI, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s