TEMDO yaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ofisi ya Kilimo na Kiwanda cha Kiteto, Manyara. Mgeni rasmi kwenye ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi wa TEMDO (Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organization) Prof. Eng. Frederick .C. Kahimba ambaye alikuwa akimwakilisha Naibu Waziri wa Viwanda Na Biashara Mh. Stella Manyanya.
Lengo ilikuwa kutembelea shamba letu la kiteto matui na kuona pia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda. Akitembelea ofisi hizo Prof. Eng. Frederick .C. Kahimba amefurahishwa kwa ujenzi huo wa ofisi kwani utaongeza tija kwa wakulima.
Ujenzi wa ofisi za JATU matui-kiteto unaendelea na umefanikiwa kufikia hatua za mwisho ambapo mpaka sasa ni vyumba vitano tayari vinajengwa kwaajili ya mkuu wa miradi, watu wa utafiti pamoja na mlinzi. Aidha baada ya ujenzi wa ofisi utafatia ujenzi wa nyumba zakuishi wafanyakazi na kutakuwepo na huduma zote muhimu, nyumba hizo zitawasaidia kuwa karibu na mradi wa kilimo. Hata hivyo baada ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi kutajengwa godauni kubwa la kuhifadhia mazao mbalimbali yatakayolimwa hapa Matui -kiteto.
#limabilastress
#2020wekezanajatu
#Investwithjatu2020
Good job JATU Team
LikeLike