FAHAMU KINACHOENDELEA SASA KWENYE KILIMO CHA ALIZETI NA JATU KITETO, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Habari,

Tunapenda kuwajulisha wanachama wote walioshiriki mradi wa kilimo cha alizeti na JATU Kiteto, Manyara kuwa tayari tumefanikiwa kufikia hatua nzuri kwani tayari mashamba yote yamepandwa na baadhi ya mazao yameshaanza kutoa matawi. Zoezi la upandaji mbegu lilichelewa kidogo kutokana na mvua zinazoendelea nchi nzima kuathiri ratiba kwani mbegu za alizeti hazipendi mvua nyingi hasa wakati wa upandaji.

Timu yetu ya maafisa kilimo na watafiti wanaendelea na zoezi la kukagua mazao ambayo yameshaanza kutoa matawi ili kuendelea kujiridhisha kuwa yanaendelea kukua kwenye ubora ili kuleta mavuno yenye tija kwa wanachama. Kilimo cha JATU ni njia pekee inayomrahisishia mwanachama kuwa mkulima pasipo yeye kupata usumbufu huku akiendelea na shughuli zake za kiuchumi na JATU ikisimamia kilimo chake. Tumejidhatiti kuhakikisha tunaleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo kwa kutekeleza kilimo cha kisasa na kinachoendana na teknolojia. Tanzania ya viwanda inawezekana tukizidi kujiimalisha kwenye kilimo cha kisasa na viwanda vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani na uchumi wa nchi yetu.

JATU – Jenga Afya Tokomeza Umasikini (Lima Bila Stress na JATU)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s