Habari,
Tunaendelea kuwajulisha wanachama walioshiriki mradi wa kilimo cha mpunga kuwa tunaendelea na hatua mbalimbali kwenye kilimo cha mpunga shambani Mbingu ambapo baada ya kumaliza hatua ya ngolezi na kupulizia madawa ya kuua magugu sasa timu yetu ya wataalamu inaendelea na zoezi la kuweka mbolea pamoja na ufuatiliaji wa kugundua magonjwa mbalimbali ambao yanaweza kujitokeza na njia za kuyakabili.
Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwenye maeneo mengi nchini hasa mvua nyingi ambazo zimeanza kuanzia mwishoni wa mwaka jana mashamba yetu yaliathiriwa mwanzoni tu mwa msimu ambapo yalichelewesha zoezi la upandaji mbegu ila kwa hatua ambayo mazao yetu yamefikia mvua nyingi hizi huambatana na magugu yanayoleta wadudu waharibifu wa mazao hivyo tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mazao yetu yanakua kwenye ubora bila kuharibiwa na magonjwa. Tumefanikiwa kupambana na hizo changamoto kwa kuhakikisha timu ya wataalamu wameweza kusaidia mabadiliko haya kwa kuchimba mifereji, kuweka matuta makubwa ya kuzuia maji na kuweka dawa za kuendelea kuua magugu.
Bado hatujapata hasara na hatutarajii kupata hasara kutokana na hizi mvua kwani tumeshajipanga kwa kuzingatia ushauri kutoka kwa watafiti pamoja na wataalamu wa kilimo ambao wako ndani ya kampuni yetu ya Jatu.
Wakulima wanaolima na Jatu wametakiwa kutegemea mavuno mengi zaidi ya msimu uliopita kutokana na vifaa vya kisasa kuongezeka pamoja na hali ya mazao ilivyo kwasasa ni nzuri sana.
Naomba kufahamu namna ya kujiunga nanyi katika kilimo cha mpunga Morogoro
LikeLike
Hello Winfrida,
Kujiunga kwenye kilimo cha mpunga wasiliana nasi 0658126324, karibu sana
LikeLike