Habari,
Tunaendelea kuwajulisha wanachama walioshiriki mradi wa kilimo cha mahindi kuwa tunaendelea na hatua mbalimbali kwenye kilimo cha mahindi shambani Kiteto ambapo baada ya kumaliza hatua ya palizi sasa timu yetu ya utafiti inaendelea na uchunguzi wa kina kugundua magonjwa mbalimbali ambao yanaweza kujitokeza na njia za kuyakabili.
Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwenye maeneo mengi nchini hasa mvua nyingi pia huambatana na wadudu waharibifu wa mazao hivyo tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mazao yetu yanakua kwenye ubora bila kuharibiwa na magonjwa. Tumefanikiwa kupambana na hizo changamoto kwa kuhakikisha timu ya wataalamu wameweza kusaidia mabadiliko haya kwa kuchimba mifereji na madawa ya wadudu.
Bado hatujapata hasara na hatutarajii kupata hasara kutokana na hizi mvua kwani tumeshajipanga kwa kuzingatia ushauri kutoka kwa watafiti pamoja na wataalamu wa kilimo ambao wako ndani ya kampuni yetu ya Jatu.
Wakulima wanaolima na Jatu wametakiwa kutegemea mavuno mengi zaidi ya msimu uliopita kutokana na vifaa vya kisasa kuongezeka pamoja na hali ya mazao ilivyo kwasasa ni nzuri sana.
Hongereni Sana Team JATU Kilimo kwa kazi nzuri ya kuongeza vifaa vya kisasa ili kuongeza mavuno kwetu cc wanachama. Mungu awabariki Sana.
LikeLike