Watumishi wa ofisi ya PSSSF Temeke wamejitokeza kwa wingi katika semina ilioandaliwa na timu ya masoko ya kampuni ya JATU iliyopo Posta jengo la PSSSF House ghorofa ya 6 na kufahamu fursa mbalimbali zilizopo ndani ya kampuni. Wamefurahia sana huduma zitolewazo na kampuni ya JATU hasa ikiwa na lengo la kuwawezesha watanzania kuzitumia fursa za kilimo cha kisasa, viwanda, mikopo na masoko ya bidhaa za chakula huku wakipata gawio kila mwezi. Hakika ile ndoto ya watanzania ya kujenga afya na kutokomeza umasikini inaenda kutimia kupitia mpango kazi ambao JATU imejipanga kwa kushirikiana na watumishi hao.
Semina hiyo ilifanyika jumanne ya tarehe 03/03/2020 na kuongozwa na Ndg. Hussein Msemwa ambae ni msaidizi mkuu wa idara ya masoko na mahusiano ya umma pamoja na wasaidizi wake.
Katika semina iliyofanyika katika ofisi za PSSSF Temeke zinazopatikana kwenye jengo la PSSSF House mtaa wa samora Posta kupitia mwakilishi wao ambae ni Ndg. Joel Mnong’one na kuweza kuongelea fursa zilizopo ndani ya Jatu zikiambatana pamoja na elimu ya uwekezaji kwenye miradi mbalimbali ya kilimo inayoendeshwa na kusimamiwa na kampuni ya JATU pamoja na programu ya kula ulipwe ambayo inaendelea kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Aidha watumishi waliohudhuria semina hiyo wamefurahishwa na semina hiyo na kusema kwamba elimu kuhusu uwekezaji na JATU ziendelee kutolewa kwa watumishi wa ofisi zingine mbalimbali na watanzania wote kiujumla kwani kampuni ya JATU ni kampuni ya kipekee sana yenye malengo ya kumkomboa mtanzania kutoka kwenye umasikini wa kipato huku akijenga afya yake kwa bidhaa bora zinazozalishwa na viwanda vya JATU.