NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE. OMARY MGUMBA AMEWAPONGEZA JATU NA VIJANA WENGINE WANAOJIHUSISHA NA KILIMO KWA KUENDELEA KUKUZA UCHUMI WA NCHI BILA KUTEGEMEA KUAJIRIWA, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

“Vijana wa sasa hivi wasibweteke tena kwani kilimo ndio ajira yenyewe, kwanza kilimo kinafaida nyingi tofauti na kuajiliwa kwani unaweza kupata chakula cha uhakika pia unatengeneza kipato kupitia biashara ya mazao” amesema Mheshimiwa Mgumba, na pia alipitisha maazimio ambayo yalipendekezwa na vijana, kuhusu kurahisisha utoaji wa mikopo kwa vikundi vya vijana kupita halmashauri.

Kwa mujibu wa serikali kila halmashauri mapato yanayopatikana asilimia kumi inatakiwa kutolewa kama mikopo kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu ili kuwawezesha mitaji ya kuanzisha na kukuza biashara au mawazo yao ya kibunifu.

Hili ni kongomano linalohusisha serikali, wadau mbalimbali wa kilimo, na vijana wa maeneo husika ili kusikiliza changamoto wanazokutana nazo vijana na pia kuonyesha fursa mbalimbali zinazofanywa na vijana wakitanzania kwa mfano JATU wameweza kukifanya kilimo kuwa fursa, ndani ya miaka mitatu wameweza kukua na kasi hadi kuingia kwenye viwanda na kutoa mikopo isio na riba kwa wakulima hii inaonesha kwa hualisia kuwa kilimo kinaweza kutukomboa watanzania kama tukukichukulia ni biashara. Pia ni vyema kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana katika suala zima la kilimo ili kuweza kuhamasisha vijana wengi wanaochukulia kilimo kama ni kazi ya wazee au ya watu masikini.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s