MRISHO MPOTO BALOZI WA JATU AWAHIMIZA WATANZANIA KUJIUNGA NA JATU PLC ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI KUPITIA KILIMO NA CHAKULA, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Balozi wa kampuni ya Jatu msanii maarufu Mrisho Mpoto amewahimiza watanzania kuzichangamkia fursa zinazotolewa na JATU hususani kwenye kilimo. Akizungumza katika kipindi chake kinacho rushwa TBC Mpoto amesema ukitaka kuwa mwekezaji mzuri na kuwekeza bila stress kampuni ya Jatu ndio kampuni wezeshi na mkombozi katika uwekezaji.

Aidha Mpoto amewataka pia watanzania wote na wawekezaji wa aina tofauti kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 14.03.2020 kwenye JATU SUPER DINNER ambao litakuwa ni tukio la aina yake ambalo limelenga kuleta maendeleo na mapinduzi katika kilimo cha kisasa cha umwagiliaji. Kupitia fursa ya mradi mkubwa wa umwagiliaji ambalo litafanyika Serena hotel Dar es salaam ambayo itakuwa na kauli mbiu ya ‘Wekeza na JATU kiteto 2020”.

Mpoto ameelezea kuwa ukjiunga na Jatu utapata faida nyingi, kwanza ni kwenye chakula ambapo inakusaidia kujitengenezea kipato kila mwezi kupitia kununua bidhaa za chakula huku tukijenga afya zetu lakini pia hufikisha bidhaa hizo mpaka walipo wateja hivyo kuwapunguzia usumbufu, pili kampuni ya Jatu inasimamia shamba na mazao yako huku wewe ukiendelea na shughuli zako iwe umeajiliwa au mjasiriamali pasipo usumbufu wowote. Lakini pia kupitia kampuni ya Jatu mkulima hatokuwa na wasiwasi wa kupata soko kwani Jatu inamsaidia mkulima kupata soko la uhakika la mazao yake ndio maana tunasema “unalima bila stress”.

Hata hivyo kwa upande wa kilimo cha umwagiliaji Kiteto Mpoto amesema, kwa njia ya umwagiliaji mkulima hunufaika kwa kupunguza gharama za kilimo na kuokoa muda kwa kutosubiri mvua za msimu. Hivyo basi hupata muda mwingi wa kushiriki shughuli zingine za kilimo cha kisasa. Pia kupitia njia hii, mkulima anakuwa na uhakika wa kupata mavuno ya kutosha kutokana na uwepo wa maji ya uhakika kwa ajili ya mimea husika hivyo kustawisha mazao yote kwa muda mfupi.

Kilimo cha umwagiliaji kiteto kitakomboa sana wakulima maana mkulima atakuwa na uwezo wa kulima mara tatu kwa mwaka na kuingiza faida nyingi kupitia kilimo hicho. Nadiliki kusema kampuni ya Jatu ndio kampuni bora kwa sasa inayo msaidia mkulima kulima kisasa kwa kusimamiwa shamba lake, kupata mkopo wa kilimo usio kuwa na riba huku akiwa na soko la uhakika la mazao yake.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s