Wakazi wa Dodoma wamejitokeza kwa wingi katika semina ilioandaliwa na timu ya masoko ya kampuni ya Jatu iliyopo tawi la Dododa mjini na kufahamu fursa mbalimbali zilizopo ndani ya kampuni. Wamefurahia sana huduma zitolewazo na kampuni ya JATU hasa ikiwa na lengo la kuwawezesha watanzania kuzitumia fursa za kilimo cha kisasa, viwanda, mikopo na masoko ya bidhaa za chakula huku wakipata gawio kila mwezi. Hakika ile ndoto ya wanadodoma kujenga afya na kutokomeza umasikini inaenda kutimia kupitia mpango kazi ambao JATU umejipanga kwa kushirikiana na wakazi hao.
Semina hiyo ilifanyika leo na kuongozwa na Rebecca Joseph ambae ni meneja rasirimali watu pamoja na wasaidizi wake.
Katika semina iliyofanyika katika kijiji cha Ng’ong’ona kupitia mwakilishi wao ambae ni ndugu Suleimani Mohamed na kuweza kuongelea fursa zilizopo ndani ya Jatu zikiambatana pamoja na elimu ya uwekezaji kwenye miradi mbalimbali ya kilimo inayoendeshwa na kusimamiwa na kampuni ya JATU pamoja na programu ya kula ulipwe ambayo inaendelea kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Aidha wanachama waliohudhuria semina hiyo wamefurahishwa na semina hiyo na kusema kwamba elimu kuhusu uwekezaji na JATU ziendelee kutolewa kwa kila mwananchi na wakazi wote wa Dodoma kwani kampuni ya jatu ni kampuni ya kipekee sana yenye malengo ya kumkomboa mtanzania kutoka kwenye umasikini wa kipato huku akijenga afya yake kwa bidhaa bora zinazozalishwa na viwanda vya JATU.
JATU~ Jenga afya tokomeza umasikini