Wanachama wakipokea kadi za bima ya afya kupitia Jatu Saccos, endelea kufuatilia blog yetu kwa taarifa zaidi

Baadhi ya wanachama wakionyesha furaha wakati wanapokea bima ya afya toka Nia njema kupitia Jatu Saccos.

Bima hii ya afya ni bima ya nia njema ambayo imebuniwa na kuratibiwa na Acclavia Insurance Brokers na kupewa dhamana na strategies pamoja na Sanlam.

Aidha bima hii pia ni ya mpango wa matibabu kwa vikundi zikiwemo saccos na ikiwa na ada ya Tsh 230,000 kwa mwaka ikiwa ni ya familia yenye watu wanne yaani baba, mama na watoto na kwa kila mtoto anayeongezeka atatakiwa kulipia kiasi cha Tsh 80,000.

Bima hii ni kwaajili ya vikundi pekee na idadi ya familia kwa kikundi ni kuanzia kaya kumi na zaidi pia umri wa mwanachama kujiunga ni chini ya miaka 64 na mtoto ni chini ya miaka 18.

Pia huduma hii isizidi watu sita ambayo ni baba, mama na Watoto, kwa upande wa magonjwa sugu kama vile cancer, sukari, mazoezi tiba n.k muda wa kusubiria ni miezi 12 pamoja na huduma ya kujifungua inachukua muda wa miezi 9.

Hata hivyo kwa upande wa mafao ya matibabu amesema kwa mwaka mgonjwa kulazwa ni Tsh 3,000,000 mgonjwa wa nje 450,000 na kujifungua kwa kawaida atalipia kiasi cha Tsh 600,000, ambapo mwanachama akiwa na bima hii ataweza kuingia moja kwa moja kwenye bima ya Maisha yaani Nia njema upande wa njiwa.

Lakini pia mafao yake ya maisha ikiwa vitatokea vifo ni kiasi cha Tsh 3,000,000 kwa mwanachama na 1,500,000 kwa mwenza na 700,000 kwa mtoto.

Matibabu hayo ni wadi/kitanda, ICU na ICCU, upasuaji, dawa maalum, vifaa vya tiba, X-ray, ultrasound, CT-scan, MRI, Densitomery scan, magonjwa endelevu, UKIMWI, kansa, Magonjwa ya kinywa, shingo na mazoezi tiba pamoja na magonjwa ambukizi.

4 thoughts on “Wanachama wakipokea kadi za bima ya afya kupitia Jatu Saccos, endelea kufuatilia blog yetu kwa taarifa zaidi

    1. Hello Frank,

      Ndio unaweza kujiunga kwa kupitia simu yako ya mkononi download application ya Jatu kwenye simu yako kisha jisajili sehemu ya sponsor na agent utajaza namba AB-2639 na AA-6086 kisha ukikamilisha usajili wako utapata namba ya uanachama ambao utakusaidia kuingia kwenye account yako ya JATU kupitia jatu app kwa taarifa zaidi unaweza tupigia kwa simu yetu namba 0688256600 au fika ofisi zetu zilizo karibu nawe

      Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s