CLOUDS MEDIA NA WADAU WA MAENDELEO NCHINI WAUPONGEZA UONGOZI WA KIMKAKATI WA JATU PLC KWA KUWAWEZESHA WATANZANIA KWENYE KILIMO CHA KISASA, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Mapema leo kampuni ya JATU ilikua mubashara katika The Big Breakfast 2020 na kituo cha habari cha Clouds Media Group yenye kauli mbiu “Uongozi wa Kimkakati”.

Akiongea katika tukio lililofanyika mapema leo asubuhi Serena Hotel Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Bw. Joseph Kusaga amesema, “Siku ya leo nina uhakika kuwa ni siku ambayo vijana wengi watafunguliwa kifikra kupitia The Big Breakfast ambapo lengo kubwa ni kusaidia vijana wa kitanzania waanze kufikiri kuhusu uongozi wa kimkakati.

Unapokuwa kiongozi wa kimkakati watu hawakufati wewe wanafata dira yako na kuhakikisha inatimia hata usipokuwepo hivyo vijana wanatakiwa kubadilika kifikra na kuweza kutumia kauli mbiu hii ya 2020, Uongozi wa kimkakati”.

Kwa upande wa Meneja Mkuu wa kampuni ya JATU Ndg. Issa Mohamedi Simbano kampuni inayojishughulisha na masuala mazima ya Kilimo, Viwanda, Masoko na Mikopo  amesema, “Kampuni ya JATU imekuja na mfumo wa kimkakati zaidi yaani kilimo biashara ambacho kitamshirikisha mtanzania kuweza kujikwamua kwenye kilimo cha mazoea na kufanya kilimo cha kisasa, yaani tunakutafutia namna ya kumiliki ardhi kwa kupitia uongozi wa JATU PLC wanasheria, maafisa kilimo tunaenda maeneo rafiki huko mikoani Manyara, Tanga n.k nakuangalia maeneo ambayo tunaweza kufanya kilimo cha mahindi, alizeti, maharage, mpunga huku usimamizi wa mashamba ukiwa chini ya wataalamu wa JATU PLC. Pia JATU inamaliza tatizo la mitaji ya kilimo kupitia mikopo isio na riba ya kilimo ambapo mkulima atachangia asilimia 30 ya gharama zote na kampuni kupitia JATU SACCOS itamkopesha asilimia 70 bila riba yoyote hivyo kufanikisha kilimo bila stress zozote za kupata mitaji na atalipa baada ya kuvuna mazao yake.

Pia mkulima anaye lima na JATU atapata soko la uhakika la mazao yake na kumsaidia mkulima kuepukana na mfumo wa madalali wengi kwa kuuza mazao yake kwenye viwanda vyetu ambavyo huchakata malighafi hizo na kuandaa bidhaa ambazo huuzwa kwa walaji wa mwisho hivyo kumsaidia mkulima kutoka kwenye kilimo cha mazoea na kuingia kwenye kilimo cha uwekezaji kwa kumiliki mnyororo mzima wa thamani kwenye biashara ya kilimo”.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s