TANGAZO MAALUMU KWA WANACHAMA WA JATU, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Habari, Tunapenda kuwatangazia wanachama wote wa Jatu na ambao sio wanachama wanategemea kuwa miongoni mwa familia ya Jatu, kumekuwa na uvumi wa taarifa ambazo sio sahihi, zikihusisha uwekezaji na ulipaji fedha wa madawa ya kilimo na uchimbaji wa madini. Taarifa hizi hazina ukweli wowote ule na Jatu haiwatambui hawa watu na hawana mikataba yoyote au ushirikiano wa kibiashara baina yao na kampuni.

Kampuni inatoa onyo kali kwa wanachama na kuwatahadharisha kwamba usitume fedha kwa namba ya simu ya mtu yeyote yule kama sio namba ya kampuni au Akaunti namba za Benki za Jatu Plc kwa ajili ya usalama wa fedha zako. Matukio haya huendeshwa na baadhi ya wanachama ambao wanatoa taarifa kwa watu na kutumia namba ambazo hazipo jatu, nazo ni kama inavyoonekana hapa chini na majina yao; –

• 255689377339 Hassan Rashid Mpera

• 255675293717 Joseph Msangi

• 255682379036 Mohamed Boko

• 255682379048 Bakary Mtego

• 255788472209 Mohamed Ismail Kusaga

• 255652599610 Jonas Maulya

Nukuu ya maneno wanayotumia watu hawa inaonyesha hapa chini; –

‘‘habari tulikuwa wote safari ya kiteto mimi ni mwanachama mwenzio na ni mmoja ya wawekezaji mkubwa jatu na nafahamiana na ndugu isare na nahusika kwenye mradi wa umwagiliaji upande wa madawa’’

‘‘habari jatu imedhamiria kuwekeza pia kwenye madini na itatumia kampuni yetu hivyo anza kuweka fedha za kununua hisa mapema katika kampuni yetu ikiwa kama wewe ni mwanachama wa Jatu’’

Mwisho kampuni inaomba ushirikiano wa hali ya juu sana kutoka kwa wanachama wote pindi utakapopokea taarifa ambayo unahisi sio sahihi au inafanana na hizo tajwa hapo juu usisite kuwasiliana nasi.

‘‘Jatu, Jenga Afya Tokomeza Umasikini’’

Imetolewa na;

Moses Lukoo William

Afisa Habari na Mawasiliano, JATU

Dar es salaam.

22 Januari 2020

One thought on “TANGAZO MAALUMU KWA WANACHAMA WA JATU, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

  1. Ni kweli hata mimi nlishangaa baada ya kuzipata hizo habari kutoka kwa mwanachama mwenzangu kuwa alipigiwa cm na mmojawapo wa hao watu wanaojitambulisha kama viongozi wa JATU na kumwambia walikuwa wote safari ya Kiteto kwahiyo watamtembelea nyumbani ili kutathmini safari !!

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s