Tunaendelea na hatua mbalimbali za mradi wa kilimo cha Mpunga Mbingu Morogoro tumeanza maandalizi ya kupanda mwezi Desemba hata ivyo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuwepo kwa mvua nyingi ilitufanya tusimamishe zoezi kwa muda na sasa, tunaendelea kupanda kwenye maeneo ambayo tulikua hatujamalizia kupanda. Sehemu ambazo tulikua tumeshapanda mpunga umeshaanza kuchipua.
Hali ya hewa ni shwari kabisa hivyo tunategemea kumaliza zoezi la kupanda mapema sana na kuendelea na hatua nyingine. Watumishi wetu wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha zoezi hili linakamilika kwa wakati ili tuweze kufikia malengo tuliojiwekea kwa msimu huu wa kilimo cha mpunga. Tunaendelea kuwahimiza watanzania wengine kuitumia fursa ya kilimo cha JATU ambacho hakina usumbufu wowote na chenye tija ili waweze kujenga afya na kutokomeza umasikini.