MUHTASARI NA MREJESHO WA KILIMO CHA MACHUNGWA NA JATU MUHEZA, TANGA

Habari,

Tunawapongeza kwa kuendelea kusubiri maelezo ya kilimo cha matunda na Jatu. Muda sasa Umefika wa kuanza mjadala wetu, naomba tuzingatie yafuatayo;

1. Jatu tunafanya kilimo kwa kumsaidia mwanachama wetu amiliki shamba, tunahakikisha unapata shamba zuri kwa bei nafuu, unapata mkopo nafuu wa kilimo usio na riba, tunakuhakikisha usimamizi wa kitaalamu katika shamba lako, mazao yote yanayopatikana katika mazao ambayo Jatu tunasimamia tuko tayari kuyanunua kwa bei nzuri ambayo haimuumizi mkulima. Tunatamani kuona jatu inalima mazao mbalimbali kwa kushirikiana na wanachama wetu. Mkulima wa jatu analima bila stress na lengo ni kujenga afya na kutokomeza umaskini.

2. Tayari Jatu hadi kufikia sasa inalima zao la mahindi, mpunga, Alizeti na maharage. Pia tunasindika na kuzalisha bidhaa zitokanazo na hayo mazao. Kwa sasa Jatu tumeamua kuingia katika zao la matunda. Tutaanza kwa kulima matunda, tutauza matunda na tutajenga viwanda vya kuzalisha juice au vinywaji kutokana na hayo matunda.

3. Kabla ya kuanza mradi wowote, tunafanya utafiti na tukijiridhisha kwamba mradi huo unaowezekana kwa faida ya kampuni na mkulima basi tunawashirikisha wanachama wetu na kuwapa mrejesho wa utafiti wetu ukiambatana na mkakati katika zao hilo. Hivyo basi kwa zao la matunda, jatu tayari tumeshafanya utafiti na tumepata majibu. Tuko tayari kufanya mradi wa matunda na tunaanza na matunda Aina ya CHUNGWA kwa mkoa wa Tanga.

4. Hapa tumeambatanisha mhutasari wa mrejesho wa utafiti tuliofanya katika zao hili. Tunaomba kila mmoja wetu asome na kuelewa kuhusu mradi huu kupitia huo utafiti. Ni hiari ya mwanachama kushiriki katika mradi huu. Soma uelewe uchambue na kutafakari ukiona yafaa changamkia fursa. Kwa wale watakao hitaji kumiliki shamba kwa kununua kupitia Jatu, tayari ekari 500 zipo kwenye app ya jatu, Nenda kaweke oda ulipie kabla hazijaisha maana tunaanza na hizo tu na awamu nyingine itakuja baada ya miaka mitatu.

5. Mjadala kuhusu kilimo cha matunda na jatu uanaendelea katika group la whatsapp la kilimo cha matunda jatu, ni group namba 1,2,3, na 4 ya kilimo cha matunda ndo mjadala wa maswali na majibu utafanyika. Kama hujajiunga wasiliana na admin akuunge kwenye moja ya hayo magroup ili usipitwe na maelezo zaidi.

Bonyeza link ifuatayo kujiunga kwenye group la kilimo cha machungwa na JATU https://chat.whatsapp.com/LLTRtzFfX63Bb9TMW1zwlT

Karibuni sana JATU,
Niwatakie heri ya mwaka mpya 2020.

Download mrejesho wa kilimo cha machungwa hapa chini

KWA HABARI ZAIDI ENDELEA KUTEMBELEA BLOG YETU

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s