MKUTANO MAALUMU WA WANAJATU DAR ES SALAAM WAFUNGUA FURSA MPYA KWA MWAKA 2020

JATU PLC imefanya mkutano maalumu na wanachama na wadau wa maendeleo nchini ambao ulikua na mambo kadhaa ikijumuisha;

1. Kujadili miradi na kampeni mbalimbali zilizojiri ndani ya JATU kwa mwaka 2019 na mafanikio yaliyopatikana

2. Uzinduzi rasmi wa programu maalumu ya masuala ya kifedha inayojulikana kwa jina la JATU PESA

3. Kupata mrejesho wa utafiti wa kilimo cha machungwa Muheza, Tanga

4. Mchakato wa kilimo cha umwagiliaji Kiteto na soko la hisa DSE

5. Kupitisha kanuni mpya za kilimo na JATU PLC

Hakika kila aliehudhuria alifurahishwa na namna ambavyo JATU imejipanga kuyainua maisha ya watanzania hasa kupitia huduma zake za kilimo, viwanda, mikopo na masoko. Meneja Mkuu wa JATU PLC Ndg. Issa Simbano aliweka wazi mipango ya kampuni ya kuendelea kushirikiana na watanzania kwenye kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo ikiunganisha na viwanda na masoko tukilenga kufungua fursa kwa watanzania wote huku pia tukitoa ajira kwa asilimia kubwa kwa vijana.

Pia Mkuu wa Idara ya Fedha Bi. Esther Marino alitoa maelezo ya kina juu ya uwekezaji kwenye mradi wa umwagiliaji wa Kiteto ikiwemo na hatua iliyofikia kwenye safari ya kuelekea soko la hisa DSE na kuwataka watanzania kuwa tayari kumiliki hisa za JATU zikiingia sokoni. Aidha Mkuu wa Idara ya miradi Bi. Esther Philemon alitoa mrejesho wa mikakati ya kilimo cha JATU katika maeneo mbalimbali ambayo kampuni inafanya uwekezaji huku takribani ekari zaidi ya 6000 zitalimwa na JATU kwa kushirikiana na wanachama wake kwenye mashamba yaliyopo Kilombero, Kilindi na Kiteto. Mkuu wa Utafiti Ndg. Paul Kapalata alitoa mrejesho wa utafiti wa kilimo cha matunda ambapo aliwaahidi wanajatu kuwa wamejiridhisha kuwa uwekezaji huu utakua na tija kwa wanachama na hivyo wachangamkie fursa kwani kilimo cha machungwa kinalipa sana. Mkuu wa SACCOS Bi. Asifiwe Mzava na Mkuu wa Idara ya Tehama Ndg. Moses Lukoo walielezea vyema juu ya programu mpya itayosaidia masuala ya kifedha ndani ya JATU maarufu kama JATUPESA ambayo itasaidia wanachama kuweka kuweka akiba na kuomba mikopo kirahisi pasipo usumbufu wowote huku ikitoa huduma mbalimbali za kifedha.

Mwisho kabisa Mkurugenzi mtendaji wa JATU PLC Ndg. Peter Isare alihitimisha mkutano kwa kujadili kanuni za kilimo na JATU ambapo kwa pamoja na wanachama walifikia muafaka wa masuala mbalimbali ambayo yatasimamia makubaliano kati ya mkulima wa JATU na kampuni huku pia yakilenga kusaidia wanachama kupata chakula kwa faida na kirahisi kupitia mifumo ya masoko na mauzo ya JATU.

JATU-JENGA AFYA TOKOMEZA UMASIKINI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s