JATU PLC yazindua ofisi zake ndani ya jiji la Dodoma ambazo zinapatikana round about ya Bahi Road jengo la Dodoma Media College ambapo tukio hilo la kihistoria liliambatana na fursa mbalimbali za Kilimo, viwanda, mikopo na masoko ndani ya JATU PLC. Wakazi wa Dodoma wamefurahia sana uwepo wa ofisi za Jatu mkoani kwao na kuahidi kushirikiana na kampuni ili dhima ya kujenga afya na kutokomeza umasikini kwa wakazi wa Dodoma ifanikiwe.
#JATUnifursaisionakikomo
#Jengaafyatokomezaumasikini