MREJESHO WA KILIMO CHA MPUNGA JATU

Kilimo cha Mpunga ni kilimo muhimu sana katika kampuni ya Jatu. Jatu tunalima mpunga kwa kushirikiana na wanachama wetu katika mkoa wa Morogoro wilaya ya kilombero.

Kituo cha jatu kinachoratibu mradi huu ni kituo cha Mbingu, Jatu kilombero branch.

Maandalizi ya kilimo cha Mpunga Jatu yana hatua zifuatazo;

1. Kukodi mashamba

2. Kuweka akiba

3. Kuanza kulima mashamba hatua ya kwanza yaani kukatua

4. Kulima mashamba hatua ya pili yaani kupiga haro au kuchabanga

5. Kupanda

6. Kupiga dawa

7. Ng’olezi

8. Kupiga dawa

9. Kuweka mbolea ya kukuzia

10. Kuvuna

Kwa mujibu wa hatua hizo, mkulima anafanya hatua ya kwanza na ya pili kwa kulipia gharama. Jatu tunaanzia hatua ya tatu. Katika hatua ya tatu Jatu inahudumia mashamba yote yale ambayo ni ya kukodi na kumiliki au ya wanachama wenyeji wote ambao wapo katika mradi wa Jatu.

Kwa mujibu wa ratiba ya mwaka huu tuliyotoa, tulionesha kwamba tutaanza zoezi la kulima mwezi November na kweli tunamshukuru Mungu tulianza tarehe 09 November zoezi la kuandaa mashamba hatua ya kwanza. Hadi kufikia sasa tumefikia zaidi ya asilimia 80 katika kuandaa mashamba. Tulitegemea kumaliza ndani ya mwezi mmoja ila zoezi limechelewa kutokana na sababu zifuatazo;

1. Tuliruhusu watu waendelee kukodi mashamba baada ya kuona hatujafikisha kiwango tulichohitaji kwa matumizi ya mwaka kesho yaani demand ya mchele wa Jatu. Hivyo watu hao tumewapa nafasi wakodi kwa sasa na hivyo wanapokodi sahizi tunachukua hatua za kutafuta mashamba na kuyalipia na kuanza kuyalima mara moja. Tunategemea ifikapo mwisho wa mwezi tutakuwa tumekamilisha kabisa zoezi la kuandaa mashamba kwa zao la Mpunga.

2. Mvua za mwaka huu kwa kilombero zimechelewa, hivyo kupelekea zoezi kuchelewa kuanza. Kwa mujibu wa majira ya sasa tunatakiwa kuanza kupanda kuanzia tarehe 20 December ili kuweza kuendana sambamba na msimu wa mwaka huu.

Kwa nini ni muhimu kuzingatia muda wa kupanda?;

Ni muhimu sana kuzingatia muda wa kupanda kwa sababu zifuatazo;

1. Inakusaidia kuchagua aina ya mbegu unayoweza kupanda.

2. Inakusaidia kujua njia au namna utakayopanda mazao yako, hapa namaanisha utapanda kwa kutumia planter, utarusha mbegu au utapanda miche (kilimo shadidi) yote haya yanategemea jinsi ulivyoendana na msimu na jinsi ulivyo andaa mashamba. Kwa mfano;

Kama utamaliza kuandaa shamba lako kwa kupiga halo bado mvua haijanyesha hapo unashauriwa kutumia planter kupanda na hii ndo njia rahisi na ya kitaalamu ambayo hata JATU huwa tunatumia.

Ukichelewa kupanda mvua ikanyesha na maji kuingia shambani huwezi tena kutumia planter ya mbegu katika maji, hapo unatakiwa kumwaga au kurusha mbegu ili ziote zenyewe bila mpangilio. Njia hii sio rafiki sana kwa kilimo cha kisasa, hapa unapunguza mapato kwani mbegu nyingi hazioti kwa mpangilio na hivyo wakati wa ng’olezi lazima utumie gharama kubwa ya kupunguza miche. Lakini pia unatumia mbegu nyingi kuliko kawaida.

Lakini pia maji yakiwa mengi sana unashauriwa kutumia njia ya kitaalamu zaidi ambayo ni kupandikiza miche. Katika kupandikiza miche hapa unapaswa kuandaa shamba lako kitaalamu zaidi kwa kutumia mashine za kisasa (rotary tiller) pia lazima uwe na kitalu kizuri cha miche yako. Unaweza kutumia nguvu kazi watu au unaweza kutumia mashine maalumu ambayo inapandikiza miche kitaalamu na kwa haraka zaidi.

JATU IMEJIPANGEJE ?

Kwa sisi Jatu mwaka huu tumejipanga kupanda mbegu kwa kutumia planter na katika kufanya hilo tayari tunapitia hatua zifuatazo;

1. Kuandaa mashamba kwa kukatua kwa kutumia trekta na jembe la disc.

2. Tunarudia kuchabanga udongo kwa kutumia haro au kwa kutumia mashine maalumu iitwayo rotavator yaani rotary tiller na hii ni mashine ya kisasa kabisa ambayo Jatu tumenunua kuhakikisha tunaandaa mashamba yetu kitaalamu.

Zoezi la kukatua linachukua muda mrefu kwa sababu wastani wa trekta moja kwa masaa 24 ni kulima ekar 50, wakati kupiga harro au kuchabanga ni wastani wa ekar 150-200 kwa masaa 24 kwa trekta moja. Hii ni kutokana na ukweli kwamba tunazo mashine za kisasa zenye uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu pasipo kusumbua na tunafanya kazi usiku na mchana kwa kupokezana maoperator wa mashine.

Kwa tunavyoongea hivi sasa kikosi kazi maalumu cha kilimo tupo kilombero na tuko hatua ya pili katika kuandaa mashamba ambayo ni kupiga haro na kuchabanga. Tunategemea kuanza hatua ya tatu ya kupanda kuanzia tarehe 20 mwezi huu. Tunamshukuru Mungu mpaka sasa hatuna tatizo lolote linaonesha kutuzuia kukamilisha ratiba yetu kama ilivyo pangwa.

Hata hivyo tunawakaribisha wakulima ambao wangependa kufika shambani na kujionea namna zoezi linavyofanyika mnakaribishwa sana fikeni katika kituo cha Jatu Mbingu, kilichopo kata ya Igima wilaya ya kilombero halafu mtaweza kuelekezwa shambani kuja kushuhudia zoezi zima.

Mwisho, naomba kuwakumbusha kwamba tunalo zoezi mbele yetu la kusaini mkataba wa kilimo cha Mpunga. Hata hivyo kutokana na ukweli kwamba bado kuna watu wanaendelea kukodi shamba hadi tarehe 31.12.2019 tunaomba mtuvumilie tutasaini mkataba wetu January 2020 kwa kila mkulima, ila tu tunaomba mjue kwamba hilo haliathiri shughuli zetu mashambani na kila kitu kinaenda sawa. Pia nitumie nafasi hii kuwakumbusha wale ambao mnategemea mkopo wa Jatu Saccos Ltd hakikisha mmekamilisha vigezo vyote na kusaini mikopo yenu kwa wakati.

Mwisho, tunawatakia wiki njema ya kumbukumbu ya uhuru na sisi tunawaambia ndani ya Jatu mko huru kulima bila stress, mwambie na mwenzako JATU ni fursa isio na kikomo.

JATU-Jenga Afya Tokomeza Umasikini

———————————
Imetolewa na;
Baba Jatu
10.12.2019

4 thoughts on “MREJESHO WA KILIMO CHA MPUNGA JATU

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s