FURSA ZA JATU PLC ZAWAGUSA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA

Wakazi wa Arusha wamejitokeza kwa wingi kwenye semina ya JATU PLC iliofanyika kwenye ukumbi wa Golden Rose tarehe 07/12/2019 ambapo ilihusisha wanachama wa JATU, vikundi mbalimbali vya wajasiriamali, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa kilimo, uwekezaji na masoko ya bidhaa za chakula.

Semina hii ni muendelezo wa programu ya kuwashilikisha watanzania juu ya fursa za uwekezaji kupitia kilimo, viwanda na masoko kupitia kampuni ya JATU PLC. Wakazi wa Arusha kiujumla walikua na kiu ya kuweza kuzifahamu vyema fursa za JATU ili waweze kuzitumia vyema kujitengenezea kipato cha ziada na kuweza kutokomeza umasikini.

Dhima kuu ya JATU PLC ni kujenga afya na kutokomeza umasikini kwa watanzania wote bila kujali hali ya kiuchumi kwa kutumia chakula cha kila siku yaani bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya JATU PLC kama mchele, unga, mafuta ya alizeti, maharage n.k. Pia uwekezaji kwenye kilimo ambacho kimeboreshwa kwenye upande wa usimamizi uliobora, pembejeo za kisasa za kilimo, mikopo isio na riba na masoko ya uhakika kinaweza kuwanyanyua watanzania kiuchumi na kuwaletea maendeleo.

JATU-Jenga Afya Tokomeza Umasikini

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s