SEMINA ZA JATU ZAWAFIKIA WAKAZI WA MOSHI-HAI, KILIMANJARO

Baada ya wakazi wa Moshi wilaya ya Hai mtaa wa bomang’ombe kuhamasika kwa muda mrefu juu ya huduma za kampuni ya JATU hatimae ile kiu yao ya kukutana na timu nzima ya masoko ya JATU PLC ili waweze kuzifahamu vyema huduma za JATU imetimia.

Timu ya masoko ikiongozwa na mkuu wa idara ya Ms. Mary Chulle ambayo ilikua safarini kuelekea Arusha kwenye semina ambayo itafanyika pale Golden Rose siku ya Jumamosi tarehe 07/12/2019 imetembelea tawi la wanajatu la Hai, Bomang’ombe na kukutana na wanachama wakereketwa ambao wamefurahi sana uwepo wa semina hii ambayo imejikita kwenye kujadili fursa mbalimbali za kilimo, viwanda, masoko na mikopo ambazo zinapatikana ndani ya JATU na kuomba ziwe endelevu ili wanachama wengi zaidi waweze kufikiwa na huduma za JATU.

Semina hii ni muendelezo wa semina za JATU zinazoendelea mikoani katika matawi yote ambapo ofisi za JATU zinapatikana zikiwa na lengo la kuimalisha uhusiano wa kampuni na wateja wake pia kuzidi kuhamasisha watanzania wengine kuweza kujiunga na JATU ili waweze kunufaika na fursa zetu.

JATU-Jenga Afya Tokomeza Umasikini

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s