JATU YAANZA UTAFITI KILIMO CHA MATUNDA MUHEZA TANGA

Kampuni ya JATU PLC kwa kushirikiana na wanachama wake wanazidi kusonga mbele kwenye uwekezaji wa sekta ya kilimo cha kisasa baada ya hivi punde kuanza rasmi utafiti kwenye kilimo cha matunda zao la mchungwa wilayani Muheza, Tanga. Hatua hii imefikiwa baada ya wiki chache zilizopita Mkurugenzi mtendaji wa JATU PLC Ndg. Peter Isare kualikwa kwenye ofisi za mkurugenzi wa halmashauri Muheza na kufanya kikao na viongozi wa wilaya na kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji ndani ya Muheza.

Lengo la JATU ni kuwa na mashamba kila wilaya nchini ambayo yanaendeshwa kisasa na kuleta faida kwa wakulima wetu lakini kabla ya kuanza uwekezaji ni desturi yetu kufanya utafiti wa kina kujiridhisha ubora wa eneo la uwekezaji na uhalali wa hayo maeneo kisheria.

Timu yetu ya utafiti ikiongozwa na Mr. Paul Kapalata imeshapiga kambi wilayani Muheza na hadi sasa inaendelea na utafiti kwa kuangalia aina mbalimbali za mbegu na ubora wake, vipimo vya udongo, magonjwa, wadudu waharibifu na aina za mbolea n.k. Matokea ya utafiti huu yatafungua ukarasa mpya kwa wakulima wa JATU ambao wamekua wakihitaji kuwekeza kwenye kilimo cha matunda kwa muda sasa.

Kuanza kwa mradi huu kutafungua fursa za kiuchumi kwa wanachama wa JATU na wakazi wa Muheza kiujumla kupitia ajira mbalimbali na kuwawezesha kulima na JATU hivyo kuongeza thamani ya kilimo chao.

JATU pia imeazimia kuanzisha kiwanda cha matunda baada ya mradi wa kilimo cha matunda kufikia hatua nzuri ili kusaidia kupanua wigo wa soko kwa wakulima wataoshiriki mradi huu na wadau wengine wa kilimo cha matunda wilayani Muheza. Tunaimani kwa kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo ya kilimo, viwanda na masoko tunaweza kuongeza tija kwenye sekta hizo na kusaidia kuinua maisha ya watanzania wengi kiuchumi. Tunaendelea kukaribisha wadau wengine kushiriki kwenye fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya JATU ili kwa pamoja tuweze kujenga afya na kutokomeza umasikini.

JATU-Jenga Afya Tokomeza Umasikini

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s