FURSA KWA WAKAZI WA ARUSHA JATU INAWALETEA SEMINA JUMAMOSI YA TAREHE 07/12/2019

Fursa kwa wakazi wa Arusha kampuni ya JATU PLC ikiongozwa na timu ya idara ya masoko chini ya Meneja Masoko Ms. Mary Chulle inawaletea semina kubwa kwa wakazi wa Arusha na mikoa ya karibu itayofanyika siku ya jumamosi tarehe 7/12/2019 ukumbi wa Golden Rose kuanzia saa 3 asubuhi, lengo ni kujadili kuhusu fursa za uwekezaji kwenye kilimo cha kisasa, viwanda vya kuchakata mazao na kula kwa faida kupitia masoko ya bidhaa za JATU PLC.

Lengo la JATU ni kujenga afya na kutokomeza umasikini kupitia rasilimali watu, kilimo viwanda na masoko hivyo kupitia semina hii na nyingine ambazo zinaendelea kwenye mikoa mbalimbali nchini ni kuweza kuwapatia fursa wakazi wa maeneo hayo ili waweze kunufaika na miradi ambayo inaendeshwa na JATU ili kusaidia jamii wanachama na jamii ya watanzania kiujumla kujipatia maendeleo.

Hivyo tunawahimiza wanachama na wasio wanachama wa JATU kujitokeza kwa wingi kwenye semina hii ili waweze kujifunza ni kwa namna gani wanaweza kushiriki kwenye fursa hizi zinazopatikana kwenye kampuni ya JATU PLC na kujitengenezea kipato cha uhakika.

JATU-Jenga Afya Tokomeza Umasikini

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s