WAKAZI WA BUMBULI-TANGA WAFURAHIA UJIO WA SEMINA ZA JATU WAAHIDI KUDUMISHA USHIRIKIANO ULIOPO

Semina za JATU , Bumbuli Tanga🔥

Vijiji vifuatavyo vimeshiriki kijiji cha kwalei, kwadoe , kwakitui, soni, Baga, kwengala na Bumbuli. JATU imeahidi kushirikiana na wakazi hao ili kuwawezesha kulima kisasa bila stress na JATU, kuwawezesha kula kwa faida kupitia bidhaa za JATU na kushirikiana nao katika kupata soko la uhakika wa mazao ya kilimo na ufugaji yanayozalishwa na wakazi hao.

Semina ilifunguliwa rasmi saa 5 asubuhi na Mwenyekiti wa kikundi cha wanajatu Bumbuli kijiji cha kwalei Ndg Vicent Seng’eng’e kwa kushirikiana na katibu wa kikundi Bi Florence ambapo walitoa mrejesho wa shughuli za kikundi cha wanajatu kama kilimo na ufugaji wa ng’ombe na kuku wa kienyeji pia suala la mikopo ya kilimo na maendeleo liliangaliwa kiundani ili kuendelea kuwawezesha wanabumbuli kuongeza mitaji.

Wanabumbuli walitoa ombi lao la uhitaji wa bidhaa za jatu hasa baada ya kukamilisha vigezo vya umiliki hisa na sehemu ya ofisi ya Jatu walioiandaa kwa shughuli za kikundi kwa matumizi ya kutoa elimu ya jatu kwa wakazi wa bumbuli, kuuza bidhaa za jatu na vikao vya wanakikundi ambapo meneja masoko wa jatu Bi. Mary Chule alikagua ofisi hiyo na kuhitaji marekebisho machache yafanyike kabla ya kuanza rasmi kutumika.

Pia tulijadili namna gani ambavyo JATU na wakazi wa bumbuli tutaendelea kushirikiana kwenye kilimo cha pamoja na masoko ya mazao ya maharage, ndizi, nyanya na vitunguu ambayo wanabumbuli wanazalisha kwa wingi. Pia wanachama walipata wasaha wa kuuliza maswali mbalimbali juu ya huduma za jatu na kupatiwa majibu yake.

Pia tulijadili namna ya kuendelea kusambaza elimu ya huduma za jatu kwa wakazi wengine ili kuongeza idadi ya wanachama wa Jatu kwa vijiji vya Bumbuli ambapo wawakilishi wa Jatu kwenye vijiji vya bumbuli, soni na wengine waliahidi kuleta wanachama wengi zaidi kwani uwepo wa semina hii imeleta muamko mkubwa kwa wakazi wa bumbuli kuendelea kuiamini na kuwekeza na Jatu ili waweze kufaidika na huduma zetu.

Wanabumbuli kwa ujumla wamefurahishwa sana na semina hizi.

Jenga Afya Tokomeza Umasikini.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s