Kwenye uzinduzi wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha wanajatu Kiteto-Manyara ambapo viongozi mbalimbali wa serikali walihudhuria akiwepo na Mkurugenzi wa halmashauri ya Kiteto Bw. Tamimu Kambona ambae amepongeza juhudi za JATU katika kuwaletea maendeleo wanakiteto na wanajatu kiujumla na wakazi wa kijiji cha matui ambapo ndo mradi huo unatekelezwa kwa kuisaidia serikali kutatua kero ya maji katika eneo hilo. Kwa kuunga mkono juhudi hizo ameahidi kutoa eneo kwa kampuni ya JATU ili iweze kujenga kiwanda cha nyama ili kusaidia upatikanaji wa soko la uhakika kwa wanakiteto ambao asilimia kubwa ni wafugaji na wakulima.