Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya JATU PLC Ndg. Peter Isare akiwa na viongozi mbalimbali katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya muheza ya mkoa wa Tanga, viongozi hao ni pamoja na Mbunge wa Muheza Mhe. Balozi Adadi Rajabu, Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe. Nassib Mmbaga na Mwenyeketi wa halmashauri ya Muheza Mhe.Bakari Mhando. Lengo la mazungumzo ni namna gani ambavyo JATU PLC inaweza kuwekeza katika kilimo cha matunda (machungwa) na kuanzisha kiwanda cha vinywaji hasa maji na juisi katika wilaya ya Muheza-Tanga ambapo Uongozi wa Muheza umesema uko tayari kutoa eneo la ujenzi wa kiwanda na eneo kwa ajili ya kilimo cha kisasa.
#WEKEZA JATU LEO UWE KATIKA MNYORORO WA THAMANI.