UZINDUZI WA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KITETO WALETA TUMAINI JIPYA KWA WAKULIMA

Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya kufanya kilimo cha kutegemea mvua hatimae tarehe 16/11/2019 JATU PLC kwa kushirikiana na wanachama wake, wadau wa maendeleo ya kilimo nchini, wasanii na waandishi wa habari pamoja kiujumla walifanikiwa  kuzindua rasmi mradi wa kilimo cha  umwagiliaji  katika  ekari 500 za mashamba ya wanajatu zilizoko  Matui Kiteto. Zoezi hili la uzinduzi wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji Kiteto lilienda sawa kwa wakulima wa JATU na viongozi wa serikali kutembelea ekari 500 zilizotengwa kwaajili ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji na kupanda miti katika mashamba hayo.

Ilikua ni furaha kwa wakulima wa JATU na wanakijiji wa Matui kwani ile ndoto yao ya kufanya kilimo cha umwagiliaji inakaribia kutimia kupitia mradi huu, hivyo uzinduzi wa mradi huu ni jambo la kipekee sana kwani JATU imejipanga kuhakikisha kila mkazi wa kiteto ana nufaika na kilimo cha umwagiliaji na kuhakikisha wakazi wote wanapata huduma bora ya maji safi kwaajili ya matumizi yao wenyewe na matumizi ya mifugo yao kwani watu wa kiteto wengi wanajishughulisha na ufugaji.

Uzinduzi wa mradi utakuwa na manufaa makubwa kwa watu wa manyara kwani utazalisha mazao mengi ambayo ni adimu kupatikana na eneo hilo kwani lina asili ya nusu jangwa hivo mazao kama mbogamboga yatayozalishwa hapo shambani yatakua chachu ya upatikanaji wa mboga za uhakika kwa watu wa manyara na mikoa mingine. Mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji utahusisha mazao ya mahindi na alizeti ili kuinua vipato vya wakulima wa JATU na wakazi wa kiteto wote kiujumla. Uhaba wa chakula cha uhakika ni sehemu ya changamoto zinazowakabili wakazi wa matui kiteto kwasababu ya ukosefu wa mvua na maji yatakayo wawezesha kulima kilimo cha umwagiliaji hivyo uzinduzi wa mradi huu ni neema kubwa kwao.

Akiongea kwenye uzinduzi wa mradi huo Mkurugenzi mkuu wa JATU Ndg. Peter Isare amebainisha dhima ya kuibadilisha Kiteto ambayo ni jangwa kuwa ya kijani kupitia kilimo cha umwagiliaji na hasa uwepo wa eneo la bustani iliyopewa jina la ‘EDEN’ itakayotengenezwa kwa muonekano wa nembo ya kampuni ya JATU.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s