Baada ya kusubiri kwa takribani mwezi mzima ile safari ya wakulima wa JATU kuelekea kwenye uzinduzi wa mashamba ya mradi wa kilimo cha Umwagiliaji Kiteto, Manyara imetimia. Ijumaa ya tarehe 15/11/2019 wadau wa maendeleo ya kilimo nchini, wasanii, waandishi wa habari pamoja na wanajatu kiujumla walianza safari yao kuelekea kwenye nchi ya ahadi shamba la JATU Matui Kiteto.
Ilikua ni furaha kwa wakulima wa JATU kwani ile ndoto yao ya kufanya kilimo cha umwagiliaji inakaribia kutimia kupitia mradi huu, hivyo kuifanya safari hii kuwa ya kipekee sana kwani JATU ilijipanga kuhakikisha kila mmoja anapata huduma bora kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari.
Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali wakati wa safari kuelekea kwenye uzinduzi wa kilimo cha umwagiliaji Kiteto, Manyara
JIUNGE NASI LEO UWE MMOJA WA WANAFAMILIA YA JATU PLC.
JATU ~~Jenga Afya Tokomeza Umasikini.
#kulaulipwe#jengaafyatokomezaumaskini