Katika muendelezo wa semina za JATU kwa vikundi na wajasiliamali mbalimbali Jumamosi hii ya tarehe 09/11/2019 tulipata wasaha wa kufanya semina na wakazi wa Chamanzi ambapo tulizungumzia fursa mbalimbali za kilimo, viwanda, masoko na mikopo kupitia kampuni yetu ya JATU PLC.
Semina hii iliyo fanyika maeneo ya Chamanzi-Mbagala kwenye muungano wa vikundi mbalimbali vya kinamama na wajasilia mali wanao ishi mahali apo. Lengo ni kuhakikisha wakazi wa maeneo hayo wanajenga afya na kutokomeza umasikini kupitia fursa za Kilimo,Viwanda,Masoko na Mikopo. Pia tunawashukuru viongozi wote wa Chamanzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Chamanzi kwa ushirikiano wao tunaimani kupitia semina hizi zitawawezesha watanzania kujenga afya na kutokomeza umasikini.
JIUNGE NA JATU LEO.
1.Ulime bila stress.
2.Soko la uwakika kwa wakulima.
3.Mikopo ya bila riba kwa wakulima.
___________________
Mawasiliano zaidi:
☎️0657 779 244
Tovuti:
http://www.jatukilimo.com