MAANDALIZI YA SAFARI YA KITETO YAZIDI KUNOGA, ZIMEBAKI SIKU 3

Ikiwa tunahesabu ni siku tatu tu, zimebaki ili kufikia ile siku ya safari ambayo wanajatu walikua wakiisubiri kwa hamu yaani safari ya Kiteto sasa imewadia. Ni Ijumaa hii wanajatu na wadau wa maendeleo ya kilimo watajumuika kwa pamoja kuelekea Kiteto kuiona nchi yetu ya ahadi, kamati ya maandalizi ya shughuli hii ikiongozwa na Mkuu wa msafara Bw. Moses Lukoo imesema kuwa maandalizi ya tukio hili kwa asilimia kubwa tayari yamekamilika kinachosubiriwa ni siku husika ya tukio.

Ilikua ni ndoto ya wanajatu kuifanya kiteto kuwa ya kijani na sasa wote kwa pamoja tunaenda kushuhudia mpaka sasa hatua iliyofikiwa kutekeleza azma hii. Kuna mengi mazuri ambayo yameandaliwa kwaajili ya wageni wote wataohudhuria tukio hili la kihistoria likiambatana na mkutano wa wakulima lakini pia tutakua na chakula cha pamoja, mbuzi choma, vinjwaji vya aina zote na burudani mbalimbali kama ngoma za asili na msanii anaetamba kwenye muziki wa Bongofleva aliyekuwa kundi maarufu la Yamoto band, Enock Bella. Tukio zima litarushwa kupitia vyombo vya habari mbalimbali ili kuhakikisha umma wa watanzania haupitwi na safari hii yenye mchango mkubwa kwenye maendeleo ya kilimo nchini.

“Twenzetu Kiteto tukaione nchi yetu ya ahadi”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s