Safari ya kampuni ya JATU PLC kuelekea soko la hisa Dar es salaam(DSE) yazidi kushika kasi baada ya juzi tu kualikwa bungeni na kufanya semina na kamati ya mawaziri sasa ni zamu ya UVCCM Taifa. Leo hii JATU imepata nafasi ya kipekee kualikwa na Umoja wa Vijana CCM(UVCCM) ambapo walifanya semina na baadhi ya watumishi wa ofisi kuu ya UVCCM Taifa pamoja na Mkuu wa Utawala UVCCM Taifa Mr. Ebeneza na kuahidi kushirikiana na JATU PLC kuwawezesha watanzania kutengeneza kipato kupitia fursa za kilimo, viwanda na masoko ambazo zinapatikana kupitia kampuni ya JATU PLC. UVCCM wanaamini kuwa endapo lengo la JATU litafanikiwa tutakua tumeisadia serikali kutokomeza umasikini kwa watanzania walio wengi, hivyo kuahidi kushirikiana nasi kwa kila hatua mpaka tufikie malengo.
Tunazidi kusonga mbele ni matumaini yetu kila mtanzania atajiunga na kwa pamoja tuweze kujenga afya na kutokomeza umasikini.
UVCCM hoyeee !! JATU hoyeee !! Kwakweli JATU itatuokolea vijana wetu ambao wangeweza kuingia kwenye makundi mabaya kwakukosa ajira. Tunamuomba Mungu awafanyie wepec vijana wetu waielewe JATU na kujiunga kwa wingi.
LikeLike