MUIGIZAJI NGULI WA TANZANIA JACOB STEVEN(JB) ATHIBITISHA KUJIUNGA NA JATU

Katika muendelezo wa semina za JATU mkoani Dar es salaam ambazo zimejikita kuwahimiza watanzania kuzitumia fursa za KILIMO, VIWANDA na MASOKO, kampuni ya JATU PLC pamoja na mwigizaji Jacobo Stephen kwa jina maarufu kama JB ambaye amethibitisha kuwa JATU PLC ni kampuni ya kipekee ambayo imelenga kumuhakikishia kila Mtanzania kipato endapo akiwa mwanachama wa JATU.

JB amekua mdau wa kilimo kwa muda sasa akisimulia historia yake baada ya kuhitimu mafunzo ya JKT aliamua kujikita kwenye biashara ya mazao hasa mpunga na mahindi katika maeneo ya Kibaigwa na Kilombero kabla ya kuamua kuwekeza nguvu zake kwenye sekta ya uigizaji. Baada ya kuisikia JATU kwa mara ya kwanza alifurahi sana maana aliona ndoto zake za muda mrefu za kuwekeza kwenye kilimo zikitimia, ndipo alipoamua kushiriki semina za JATU ili kuzifahamu vyema huduma zetu na baada ya kujiridhisha aliamua kujiunga rasmi na kuwa mwanachama huku pia akiahidi kununua hisa pindi soko litapofunguliwa.

Tunazidi kuwakumbusha na watanzania wengine kujiunga na JATU ili wawe sehemu ya mafanikio ambayo kampuni imeyalenga kuwapatia wanachama wake.

JIUNGE NA JATU PLC SASA 🔥 📞0657 779 244

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s