Leo timu ya Jatu PLC ikiongozwa na Mkurugenzi wetu Ndg. Peter Isare imetembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tulipata wasaha wa kuwa na mkutano uliwahusisha Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu; Bunge, sera, ajira, kazi na wenye ulemavu, Mhe. JENNISTER MHAGAMA, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Katiba na sheria ambaye pia ndie Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mhe. Najima Giga. Pia mkutano huu ulihusisha Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge, Sheria na Katiba pamoja na viongozi wakuu wa idara ya vijana ofisi ya Waziri mkuu.
Kamati nzima imefurahishwa na ujumbe mzito kutoka Jatu na kuahidi kuendelea kushirikiana na kampuni yetu na pia kuhamasisha wabunge na mawaziri kuzitumia fursa za JATU hasa kipindi hiki tunapoelekea soko la hisa. Sisi kama JATU tunayo furaha kubwa kupata nafasi hii ya kipekee na kuwaahidi wanachama wetu kuwa tutaendelea kuipeleka JATU mbali zaidi na hatimae kutimiza malengo tuliyojiwekea. Tunaendelea kuwakaribisha wananchi wengine kuja kuwekeza JATU na kuzidi kuwapongeza wanachama wetu kwa kutuamini na kuwa nasi pamoja mpaka, JATU tunaamini penye nia pana njia ndio maana tulianza kwa kutambaa, tukasimama na sasa tunatembea tukibeba mafanikio kwa pamoja.
~JATU, Jenga Afya Tokomeza Umasikini~