TAARIFA KWA UMMA WA JATU PLC

UFAFANUZI ZAIDI KUHUSU KUPATA WADHAMINI WA MCHAKATO WA SOKO LA HISA (UNDERWRITERS) KWA AJILI YA JATU PLC

1. MAANA YA SOKO LA HISA NA MCHAKATO WAKUINGIA SOKONI:

Soko la hisa ni taasisi inayosimamia na kuratibu mchakato wa uuzaji na manunuzi ya dhamana za mitaji mfano hisa.
Kwa Tanzania kuna soko moja tu lenye dhamana hiyo, yaani Soko la Hisa la Dar es Salaam (Dar es Salaam Stock Exchange, (DSE) hili ndo soko pekee linalohusika na kukuza mtaji kwa kuuza sehemu ya umiliki (HISA) kwa Umma.

Kabla ya kufikia hatua ya kuuza hisa katika soko hili, muuzaji huwa anaandaa nyaraka mbali mbali ambazo huwa zinasomwa na kupitishwa na mamlaka husika; kwaTanzania tunayo mamlaka ya masoko na mitaji ambayo ni taasisi ya serikali inajulikana kwa kifupi kama CMSA Yaani Capital Market and securities Authority.

Kampuni inayouza hisa lazima ithibitishwe na CMSA pamoja na DSE ndipo iruhusiwe kutangaza na kuuza hisa zake kupitia soko la mitaji la Umma. Moja ya nyaraka muhimu sana katika mchakato huu ni waraka wa matarajio Yaani PROSPECTUS.

Prospectus inaandaliwa na muuzaji na moja ya vitu inavyotakiwa kuelezea ni pamoja na; mkakati ambao kampuni itatumia kufanikisha kuuza hisa na faida ambayo mwanahisa wataitarajia kutokana na uwekezaji huo. JATU PLC tayar tumefanikiwa kuandaa waraka huu na tumeweza kupeleka maombi yetu kwa mamlaka husika Yaani DSE na CMSA ili waturuhusu kuuza hisa zetu kwa Umma kupitia soko la DSE.

2. USHAURI WA DSE NA CMSA;

Moja ya ushauri ambao ulitolewa na mamlaka zote mbili kwa maana ya DSE na CMSA baada ya kusoma nyaraka zetu zote; walishauri kwamba ni vyema tuwe na UNDERWRITERS Yaani kwa lugha rahisi ni wadhamini ambao wataweza kuihakikishia mamlaka kwamba Jatu ikiingia sokoni ndani ya siku chache (si zaidi ya mwezi mmoja) itakuwa imeuza hisa zote na kukusanya mtaji wa TSHS. billion 7.5.

3. NI NANI ANAWEZA KUWA UNDERWRITER WA HISA?

Mtu yeyote mwenye pesa anaweza kuwa underwriter wa hisa za JATU, lengo la kuwa na underwriters ni kujiaminisha kwamba endapo wateja watakosa kipindi cha kuuza hisa muda tutakao pewa ukiisha basi huyu mdhamini (underwriters) anaweza kuzinunua hisa zote za JATU ili tupate mtaji wa kutekeleza mpango biashara wetu.

Kujiaminisha kuuza hisa katika soko la hisa ni jambo zuri kwa pande zote yaani kwa mamlaka inayosimamia soko na kwa kampuni inayopeleka hisa sokoni; Kwani endapo kampuni itaenda soko la hisa bila kujihakikishia kwamba inaweza kuuuza hisa zote kwa wakati uliotengwa basi kuna uwezekano mkubwa kampuni hiyo kushindwa kukidhi vigezo na hivyo kutoruhusiwa kukusanya mtaji kutoka kwa umma, lakini pia inaleta picha mbaya kwa mamlaka zinazosimamia soko la hisa Kwani soko linaonekana kudorora na hivyo kutokuvutia wawekezaji wapya.

Underwriter (s) anaweza mtu mmoja au hata zaidi ya watu 1000 na unapokuwa underwriter haimanishi kwamba wewe tayar umenunua hisa, wewe utasuburi hadi watu wanunue zile ambazo zitabaki bila kununuliwa ndizo ambazo utaruhusiwa kununua.

Anaweza kujitokeza mtu au kampuni moja tu au 2 zenye mtaji mzuri zikadhamini mchakato huu kwa maandishi (kila mmoja anasema ni hisa kiasi gani aweza Nunua incase..) na wakasubir tukiingia sokoni wateja wetu wakanunua hisa zikabaki wao wanunue na ikitokea zimenunuliwa zote kwenye soko la awali basi wao hawatakuwa na hisa za kununua tena.

Kumbuka underwriters ni watu ambao wananunua hisa katika soko la awali baada ya hisa hizo kushindwa kununuliwa na wateja wa kawaida, na baada ya hapo kampuni inaorodhesha hisa zote katika soko, ambalo kitaalamu linajulikana kama SECONDARY MARKET, katika secondary market huwa wateja wanauza na kununua hisa kwa kadri wanavyoweza na kwa bei ya soko; hivyo mtu anaweza kununua hisa wakati wa IPO (primary market) na akasubiri wakati wa soko la pili bei ikiwa imepanda akauza hisa zake na kurudisha fedha yake na hata kupata faida maradufu; swala la faida sasa inategemea na bei ya hisa kwa wakati wa kununua na wakati wa kuuza.

4. KWANINI JATU IMEAMUA KUANZA NA WANACHAMA WAKE KABLA YA KUTAFUTA WADHAMINI WENGINE WA NJE?

Uongozi wa Jatu unajivunia wanachama waliopo JATU. Uongozi unaamini kwamba shiling bilion saba na million mia tano (7,500,000,000/-) ambayo ndo jumla ya fedha tunayotegemea kuuza hisa kupitia soko la hisa ni pesa ndogo sana ambayo wanachama wa Jatu wanaweza kumudu; lakini pia uongozi wa JATU unaamini kwamba JATU ni kwa ajili ya watanzania wa kipato cha kawaida na lengo ni kuwawezesha waweze kumiliki kampuni kubwa ya kisasa na wafanye miradi jumuishi kama vile Kilimo, viwanda na masoko. Kwa sababu hizi uongozi umeona ni vyema kuanza na wanachama kwanza ili wao wajitokeze na kusema Utayari wao katika kununua hisa unakomea wapi? Yaani kwa mfano kama tunazaidi ya wanachama 10,000 na wote wakaamua kununua hisa za JATU maana yake ni kwamba bila kujali uwezo wa kila mmoja (tunajua tunatofautiana) lakini wastani wa kila mmoja akinunua angalau hisa za Tshs 750,000/= tutafikia malengo yetu bila kuhangaika na hao wadhamini.

Hivyo basi barua au tangazo lilitoka leo likihasisha wanachama waweze kuweka ahadi maana yetu ni kwamba tuwathibitishie mamlaka ya DSE na CMSA kwamba sisi wanachama wa JATU PLC tunaouwezo wa kununua hisa zote kwa bei ya Tshs 2500/= kwa kila hisa moja pindi dirisha la kuuza hisa litakapofunguliwa. Na uongozi wa jatu utaorodhesha majina yenu yote pamoja na kiasi mlicho ahidi tutawatumia mamlaka husika nao watajiridhisha ili watupangie ratiba ya kuingia sokoni.

Itambulike kwamba swala hili ni la hiari kabisa na wala hautakiwa kutoa pesa zako na kuzilipa JATU, sisi tunataka tu utuhakikishie kwamba wewe ni miungoni mwa wanachama ambao watanunua hisa, na tujue ni hisa za thamani ya kiasi gani; kitaalamu hapa tutakuwa tunajenga kitabu cha wawekezaji wapya (book building). Pia ikumbukwe kwamba utaratibu huu hauathiri umiliki wako wa awali kwa maana ya kwamba kama ulishanunua hisa za JATU hapo nyuma haimanishi kwamba zile hisa hazitambuliki, hisa zako zinatambulika na tayari orodha hiyo ipo katika mamlaka husika. Kwa sasa tunaongelea hisa mpya ambazo tunatarajia kuuza hivi karibuni kupitia soko la DSE na unaruhusiwa pia kununua zaidi kama unao mtaji.

5. NI KWANINI UNUNUE HISA ZA JATU PLC?

Wengi wenu mtajiuliza, je kuna umuhimu gani wa kununua hisa za JATU, nataka nikuhakikishie kwamba katika historia ya nchi yetu kwa mara ya kwanza imetokea kampuni ambayo inajibu hoja zote za watanzania kuhusu kupambana na umaskini, waasisi wa JATU waliamua kuanzisha kampuni hii na kuifanya iwe ya Umma kwa sababu waliamini na wanaamini ni suluhisho la umaskini na inatoa kipato kwa kila Mtanzania. Pamoja na kusudi hilo; ukinunua hisa za JATU ni tofauti na hisa zingine ulizozoea kwa sababu;

1. Mbali na gawio la faida kila mwaka(dividend), JATU inawasaidia wakulima kwa kuwatafutia mashamba, kuwapa wataalamu wa kilimo, kujenga miundombinu ya kisasa na kutoa mkopo wa kilimo usio na riba kwa mkulima; na ili uwe mkulima wa JATU ni lazima uwe na hisa angalau 400.

2. Tunao mfumo wa mabalozi ambao wanasambaza bidhaa za JATU kwa kuwauzia wateja wa JATU walio karibu nao, balozi anapata faida kubwa zaidi kutokana na Mfumo wa JATU na gawio la faida la kila mwezi; ili uwe balozi wa JATU utalazimika kuwa na hisa angalau 400.

3. Lakini pia JATU inamfumo wa masoko ambao unawezesha watu wanununue bidhaa na kuuza kupitia mtandao wake, wewe kama ni mjasiriamali utaruhusiwa kuuza bidhaa zako kwa wanachama wa JATU, hutopata shida ya soko, lakini ni lazima pia uwe na hisa JATU

4. Kubwa zaidi ni kwamba JATU inahuduma ya kifedha ambapo tunatoa mikopo kwa wanachama wetu na hawa wanachama ni lazima wawe wanahisa.

Hivyo basi; kutokana na sababu Tajwa hapo juu; kila Mtanzania mwenye nia ya maendeleo analazimika kununua hisa za JATU ili apate fursa hizo; tunaamini kwamba wapo wengine ambao watashindwa kununua hisa wakati huu wa IPO lakini hiyo ni fursa Kwa wale ambao mtanunua hisa nying, kwani mtaweza kuuza hisa zenu kwa wageni watakao kuja kwa bei mtakayotaka wenyewe hapo badae, na hii itawawezesha pia kukuza kipato chenu. Amini usiamini kuna kila dalili inaonesha kwamba hisa za JATU zitakuwa zikipanda bei na wengi wenu mtatajirika kutokana na hisa mtakazo kuwa nazo JATU PLC.

MWISHO:

Kuhusu kuwa underwriters nayo pia ni fursa, kama wewe ni mtu binafsi au taasisi ambayo inadhani kwa namna moja au nyingine unaweza kuthamini hisa hizi pia tunakukaribisha wasiliana nasi ili tuweze kuweka makubaliano bayana ya kisheria na wewe utakuwa underwriter wa hisa za JATU, Kumbuka ukiwa underwriter kuna faida au ofa unayopata ambayo ni ya upendeleo kutokana na makubaliano tutakayo ingia.

Napenda kuwashukuru kwa mapenzi mema mliyonayo juu ya Nchi yetu na sasa mmeamua kuwekeza kupitia JATU, nawashauri mfanye maamuzi sahihi baada ya kutathimini swala hili na kujiridhisha, tafadhari usitoe pesa yeyote kwa yeyote yule kwa kipindi hichi; zoezi hili sio la kuuza hisa bali ni la kutaka kujiridhisha kama tunao wanunuzi wa hisa za JATU. Weka ahadi yako kwa kadri uwezavyo; wasilisha katika ofisi husika, baada ya hapo kaa usubiri ratiba ya soko la hisa tutawatangazia hivi karibuni na wewe utaenda kununua hisa zako kwa mawakala tutakao watangazia.

MUHIMU:
Unaruhusiwa kumshirikisha rafiki yako habari hizi, hata kama sio mwanachama kwa sasa lakini anayo nia ya kuwekeza JATU, Mpe habari njema.. hata walio nje ya Tanzania pia tunawakaribisha, iwe taasisi ya Umma, vikundi, kampuni au watu binafsi njoo tuungane tuokoe Nchi yetu kwa kupambana na umaskini. Kumbuka tunauza hisa kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika kilimo ili tuasaidie watu wengi Zaidi na Kujenga kiwanda cha kisasa katika mkoa wa Manyara wilaya ya Kiteto kwa ajili ya kuzalisha unga wa mahindi na mafuta ya alizeti ambavyo ni chakula muhimu kwa maisha yetu sisi wanadamu.
___________________________________

Imeandikwa na;
Peter Isare
Founder and CEO
JATU PUBLIC LIMITED COMPANY 16.10.2019

JATU – JENGA AFYA TOKOMEZA UMASKINI

5 thoughts on “TAARIFA KWA UMMA WA JATU PLC

 1. Nimekuelewa Sana, mkurugenz
  Kwa pamoja tunaweza kujenga afya na kutokomeza Umaskini
  Na hapa ndo naiona ile dira ya JATU plc.
  “Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki JATU plc”

  Like

 2. Ushauri wangu viongozi naona mngetumia muda huu kukaa na kuhakikisha bidhaa hazipungui stoo, maana haiwezekani watu wanazunguka kutafuta wateja halafu unaingia kwenye system unakuta sembe hakuna, na wakati mwingine unakuwa tayari umeshatumiwa pesa kwenye simu so unalazimika kurudsha pesa ya watu unaingia hasara maana lazima ukatwe, lakini pia unakuwa umeshampoteza huyo mteja maana hawezi kukuamini tena. So naona kipaumbele kwanza muangalie na kuhakikisha mzigo upo wa kutosha ili iwe rahisi mtu kufanya order muda wowote.

  Like

 3. Nimepokea kwa furaha kubwa mchakato mzima wa kuuza hisa nami kama mwanachama wa JATU niko tayari kununua hisa 300. Mungu atusimamie 🙏🏽

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s