SAFARI YA WANAJATU KILIMO-KITETO IMEWADIA.. RATIBA NA MAELEKEZO YOTE YAKO HAPA

Waandaaji: JATU PLC

Wahusika: Wakulima wa JATU, Viongozi wa kiserikali, Balozi wa JATU(Mkaliwenu) na Viongozi wa JATU.

JATU PUBLIC LIMITED COMPANY ni kampuni ya umma inayowaunganisha wakulima na kuwatafutia mashamba kisha kuwawezesha wanachama kukodi au kununua mashamba, kampuni huyasimamia mashamba hayo kwa kutumia wataalamu waliobobea kwenye kilimo na baada ya mavuno kampuni hununua mazao yote na kuandaa bidhaa ambazo huuzwa kwa wanachama wa JATU kwa mfumo maalumu unaomhakikishia mteja gawio la faida kila mwezi.

Pia ni kampuni inayowawezesha wakulima kupata mikopo isiyokua na riba kwaajili ya kilimo. Kampuni hii inamiliki viwanda vya uzalishaji bidhaa mbalimbali za chakula kama vile mchele, unga wa mahindi na mafuta ya kupikia. Kampuni inasimamia mashamba makubwa ya wanachama ambayo yanalimwa mazao mbalimbali kama vile mahindi, maharage, mpunga na alizeti katika mikoa ya Manyara, Morogoro na Tanga.

Safari ya Kiteto:

Ni safari maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya JATU PLC kwaajili ya wakulima na wanachama wa JATU ikishirikisha viongozi wa kiserikali na wadau wa maendeleo ya kilimo.

Lengo:

Safari ya Kiteto ina malengo makuu matatu kama ifuatavyo:-

 1. Kushuhudia mashamba ya JATU yanayoandaliwa kwaajili ya kilimo cha kisasa (umwagiliaji).
 1. Mkutano wa wanajatu kilimo kufanya tathmini ya msimu uliopita wa kilimo na mpango kazi wa msimu mpya wa kilimo wa mwaka 2019/2020
 1. Kushirikisha serikali juu ya nia ya JATU kuboresha mfumo wa uwekezaji kwenye kilimo, viwanda na masoko

Ratiba ya shughuli nzima itakavyokua

Kundi la kwanza: Mtwara na Lindi

 • Kwa wale wanaotokea Mtwara na LIndi makutano ni ofisi za JATU Dar es salaam Sabasaba tarehe 15/11/2019 saa 7 kamili mchana na safari itaanza saa 8 kamili mchana kuelekea Kiteto wakiungana na wale wa Dar es salaam.

Kundi la pili: Dar es salaam

 • Kwa wale wa Dar es salaam makutano ni ofisi za JATU sabasaba tarehe 15/11/2019 saa 6 kamili mchana. Safari itaanza saa 8 kamili mchana kuelekea Kiteto.
 • Tutawapitia watu wa Kimara, Mbezi na kibaha njiani kisha kuendelea na safari kwa watu wa Morogoro tutawakuta stand kuu ya msamvu kwenye saa 11 jioni. Safari yetu itaendelea na kisha tutampumzika, tutapata chakula cha usiku na kulala Kibaigwa.
 • Tarehe 16/11/2019 saa 1 kamili safari yetu ya kuelekea Kiteto itaendelea na tunategemea kundi la kwanza na la pili kufika Kiteto kwenye saa 3 asubuhi.

Kundi la tatu: Mwanza

 • Kwa wale wa Mwanza makutano ni ofisi za JATU Mwanza saa 12.30 asubuhi. Safari itaanza saa 1.30 asubuhi na tutawapitia watu wa Shinyanga, Nzega, Igunga na Singida ambapo tunategemea watapumzika na kulala Dodoma.
 • Jumamosi ya tarehe 16/11/2019 kundi la Mwanza wataungana na watu wa Dodoma na saa 12.30 alfajiri safari ya kuelekea Kiteto itaanza ambapo tunategemea saa 3 asubuhi wafike Kiteto.

Kundi la nne: Arusha

 • Wale wa Arusha, Tanga na Moshi makutano ni ofisi za JATU Arusha saa 7:30 mchana na safari ya kuelekea Kiteto itaanza saa 8 kamili mchana.
 • Watalala Kiteto mjini na saa 2 asubuhi wataanza safari ya kuelekea shambani Kiteto.

Download ratiba ya safari ya wanajatu kilimo Kiteto

3 thoughts on “SAFARI YA WANAJATU KILIMO-KITETO IMEWADIA.. RATIBA NA MAELEKEZO YOTE YAKO HAPA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s