JATU YAZINDUA KULA ULIPWE, YASEMA UKOMBOZI KWA MTANZANIA WA CHINI WAJA

Kampuni ya Jatu iliyojikita katika kilimo, viwanda na masoko imesema kuwa, itahakikisha inawanufaisha watanzania wote katika miradi yake wakiwemo watanzania wa kawaida.

Hayo yamezungumzwa jijini Dar es Salaam leo Septemba 21.2019 na Mhandisi Dk. Zaipuna Yonah wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kula ulipwe inayoendeshwa na kampuni hiyo, ambapo alisema kwamba, dhamira ya jatu ni kuhakikisha Mtanzania anashikilia mnyororo wa thamani wa uandaaji wa bidhaa za chakula hata kama ni Mtanzania wa kawaida.

Akifafanua kuhusu hilo, Dk Zaipuna alisema kuwa “Kifupi tunataka Mtanzania wa kawaida apate kumiliki mnyororo wa thamani kuanzia ardhi, kulima, kuchakata, kusafirisha hadi hatua ya sokoni jambo ambalo kwa mwanachama wa jatu linawezekana kabisa”.

Aidha, Dkt. Zaipuna alieleza namna Jatu inavyowawezesha wanachama wake kula kwa faida kupitia kampeni hiyo ya kula ulipwe, ambapo amesema kuwa Jatu hugawana faida na wanachama wake kwa kila manunuzi ya bidhaa wanayoyafanya na hivyo kufafananisha kitendo hicho ni sawa na ulaji wa mwekezaji ambaye siku zote hula kwa faida.

Naye Afisa utawala wa Jatu; Bi; Esther Kiuya, amesema kwamba, kampeni ya kula ulipwe inaashiria upendo ndani yake, kwani kinachofanyika katika kampeni hiyo ni mteja kugawana sehemu ya faida ya bidhaa na kampuni kitu ambacho ni cha pekee kwani siyo makampuni yote hufanya jambo hilo.

Hata hivyo, Bi: Kiuya amewasihi watanzania ambao bado hawajajiunga na Jatu kufanya hivyo ili na wao waanze kula kwa faida , sambamba na kukamata mnyororo wa thamani katika bidhaa za chakula kupitia kushiriki miradi ya kilimo ya Jatu ambayo ni ya kisasa na yenye matokeo ya uhakika.

Pamoja na hayo, kupitia uzinduzi huo kampeni ya kula ulipwe Jatu imemtangaza rasmi balozi wao Ndugu; Jacksoni Supakila maarufu kama Mkali wao kuwa ndiye balozi wa kampuni kwasasa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s