Zoezi la kuchimba visima vya maji kwenye mradi wa JATU kilimo Kiteto lazidi kushika kasi

Hayawi hayawi sasa yamekua, ilikua ni ndoto ya wanajatu kufanya kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza tija kwenye mavuno ya mazao yao. Penye nia siku zote hapakosi njia kutokana na juhudi kubwa za viongozi na wanachama wetu sasa tunajivunia na kutembea kifua mbele kwani zoezi la kuchimba visima linaloendelea Kiteto limefikia hatua nzuri.

Zoezi hili linaloenda kwa kasi na ufanisi mkubwa, baada ya kukamilika sehemu ya kwanza, bado kama sehemu tatu za utafiti ili kumaliza zoezi hili. Wiki ijayo tutaendelea na Pumbing Test ili kujua kiwango cha maji, hii itatupa picha ya kujua ni visima vingapi tunahitaji na vya urefu gani. Hadi kufikia hapo tumeenda mita 210 japo maji yalianza kupatikana mita 138. Maji ni ya baridi kabisa hayana chumvi na ni mazuri kwa matumizi ya nyumbani na shambani, mpaka hapa tulipofikia hatuna budi kusema Asante Mungu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s