JATU YAZINDUA RASMI KAMPENI YA KULA ULIPWE MTAA KWA MTAA

Kampuni ya JATU(PLC) leo imefanya uzinduzi rasmi wa kampeni iitwayo kula ulipwe jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika kigamboni maeneo ya ferry Afisa Masoko wa JATU Ndugu Hussein Msemwa amesema kuwa kupitia kampeni hiyo watanzania wataweza kujitengenezea kipato cha ziada endapo watafanya manunuzi ya bidhaa za chakula kwa kutumia mfumo wa Jatu(JATU APP).

Aidha Ndugu Msemwa amewataka watanzania ambao bado hawajajiunga na Jatu kufanya hivyo ili waanze kunufaika na huduma bora za chakula, lakini pia waweze kupata magawio ya faida kila mwezi kutokana na manunuzi ya bidhaa wanayofanya.

Pamoja na hayo, Ndugu Hussein afisa masoko wa JATU amesema kuwa kwa sasa kampuni ya Jatu imeandaa bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na unga wa sembe na dona, mafuta ya kupikia ya alizeti, mchele, maharage pamoja na karanga ambavyo vyote hivyo mteja huweza kuvinunua kupitia JATU APP na kufikishiwa bidhaa zake mpaka mahali alipo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s