Baada ya zaidi ya miaka mitatu kwenye kilimo wilayani Kiteto sasa tunazidi kusonga mbele kwa kasi na sasa JATU imeamua kutekeleza maazimio yake ya kuja na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa lengo la kuongeza tija kwa wakulima wetu ambao wamekua nasi bega kwa bega. Tulianza kwa kufanya utafiti wa kina wa kutafuta vyanzo vya maji, ambapo tulileta matumaini mapya kwa wakulima baada ya kupata uhakika wa chanzo cha maji yaani water table. Baada ya kukamilisha zoezi la utafiti tulianza uchimbaji maji kwa kutumia mitambo maalumu ya kisasa, zoezi hili limefanikiwa na sasa kilimo cha umwagiliaji cha JATU kitaanza rasmi.
Hivyo Kampuni ya JATU PLC inayofuraha kukutangazia wewe mtanzania uliyekosa nafasi ya kumiliki shamba la umwagiliaji katika msimu uliopita, sasa mashamba yanapatikana kwa gharama ya shilingi laki saba na nusu kwa hekari moja ambapo mpaka sasa zipo hekari 500. Mashamba haya ya umwagiliaji yanapatikana kupitia APP ya JATU iliyopo play store. Kuanza rasmi kwa mradi huu ni fahari kubwa kwa wakulima wa JATU na watanzania wengine ambao wangependa kushiriki kwenye miradi ya kilimo na JATU, kwa pamoja tunasema “Kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji kinawezekana”.
Hongera sana Jatu,naona Mungu akiwapamoja nasi hakuna wakuzuiya mafanikio yetu tuendelee mbele kwa kumtumaini tuu tutafika mbali.barikiwa sanaaaaaa
LikeLike
Yes I need Shamba la kilimo kiteto
LikeLike
Habari Joel,
Kwa taarifa juu ya mashamba yetu wasiliana nasi 0657779244
LikeLike