BREAKING NEWS: TONE LA KWANZA LIMERUKA… KITETO YAGEUKA KUWA NCHI YA ASALI NA MAZIWA

Kiteto ni wilaya yenye ardhi yenye rutuba nyingi kwaajili ya kilimo japokua inakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji kutokana na asili ya eneo hilo kuwa nusu jangwa. JATU kwa kushirikiana na wanachama wake waliiona fursa ya uwekezaji nakuamua kuanzisha mradi wa kilimo cha Alizeti na mahindi, kilimo hiki kilitegemea mvua za msimu kwa miaka zaidi ya miwili tukikabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa, kitu ambacho kilisababisha mavuno kutokua lukuki. Penye mafanikio siku zote hapakosi changamoto malengo ya JATU ni kuongeza tija kwa wakulima, thamani ya kilimo kama uti wa mgongo wa mtanzania na mwanajatu kilimo kwa ujumla pia kuongeza chachu ya watanzania kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa hasa cha JATU kwani kuna faida nyingi ikiwemo kusimamiwa shamba, kupatiwa mikopo isio na riba na uhakika wa soko.

Mradi wa kilimo cha JATU na wanachama wake Kiteto ulianza rasmi mwaka 2016 ambapo tulianza na takribani ekari 1000 kwa mazao ya mahindi na alizeti. Matunda ya uongozi ulio makini na wanachama wenye kiu ya mafanikio kwenye kilimo, uwekezaji umeongezeka kwa mwaka huu hadi kufikia ekari 2,500, hivyo kufikia nusu ya malengo ya ekari 5,000 kwa mradi wa Kiteto pekee ifikapo mwaka 2022. Safari yetu haikua rahisi, tunaamini nyota njema huonekana asubuhi kwani tulipotoka sipo tulipo sasa, mabadiliko kwenye sekta ya kilimo yanahitaji uboreshaji wa miundombinu na ujenzi wa viwanda vya kutosha.

Tunazidi kusonga mbele kwa kasi na sasa JATU imeamua kutekeleza maazimio yake ya kuja na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa lengo la kuongeza tija kwa wakulima wetu ambao wamekua nasi bega kwa bega. Tulianza kwa kufanya utafiti wa kina wa kutafuta vyanzo vya maji, ambapo tulileta matumaini mapya kwa wakulima baada ya kupata uhakika wa chanzo cha maji yaani water table. Baada ya kukamilisha zoezi la utafiti tulianza uchimbaji maji kwa kutumia mitambo maalumu ya kisasa, zoezi hili limefanikiwa na sasa Kiteto sio jangwa tena bali nchi yenye asali na maziwa.

Hivyo Kampuni ya JATU PLC inayofuraha kukutangazia wewe mtanzania uliyekosa nafasi ya kumiliki shamba la umwagiliaji katika msimu uliopita, sasa yanapatikana kwa gharama ya shilingi laki saba na nusu kwa hekari moja ambapo mpaka sasa zipo hekari 500. Mashamba ya umwagiliaji yanapatikana kupitia APP ya JATU iliyopo play store. Kuanza rasmi kwa mradi huu ni fahari kubwa kwa wakulima wa JATU na watanzania wengine ambao wangependa kushiriki kwenye miradi ya kilimo na JATU, kwa pamoja tunasema “Kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji kinawezekana”.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s