JATU PLC NI NINI?

JATU PUBLIC LIMITED COMPANY ni kampuni ya umma inayowaunganisha wakulima na kuwawezesha kulima kisasa na baada ya mavuno kampuni hununua mavuno yote na kuandaa bidhaa ambazo huuzwa kwa mawakala na wanachama wa JATU kwa mfumo maalumu unaomhakikishia mteja gawio la faida kila mwezi. Pia ni kampuni inayowawezesha wakulima kupata mikopo isiyokua na riba kwaajili ya kilimo. Kampuni hii inamiliki viwanda vya uzalishaji bidhaa mbalimbali za chakula kama vile mchele, unga wa mahindi na mafuta ya kupikia. Kampuni inasimamia mashamba makubwa ya wanachama ambayo yanalimwa mazao mbalimbali kama vile mahindi, maharage, mpunga na alizeti katika mikoa ya Manyara, Morogoro na Tanga.

FURSA KWA WAKAZI WA ARUSHA JATu inawaletea semina siku ya jumamosi tarehe 7/12/2019

Fursa kwa wakazi wa Arusha kampuni ya JATU PLC ikiongozwa na timu ya idara ya masoko chini ya Meneja Masoko Ms. Mary Chulle inawaletea semina kubwa kwa wakazi wa Arusha na mikoa ya karibu itayofanyika siku ya jumamosi tarehe 7/12/2019 ukumbi wa Golden Rose kuanzia saa 3 asubuhi, lengo ni kujadili kuhusu fursa za uwekezaji kwenye kilimo cha kisasa, viwanda vya kuchakata mazao na kula kwa faida kupitia masoko ya bidhaa za JATU PLC.

jatu yashiriki maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya tanzania sabasaba dar es salaam

Jatu inapenda kuwataarifu wanachama wake kuwa tupo katika maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania, maonesho ambayo yanafanyika katika viwanja vya sabasaba maonesho barabara ya Kilwa.

Maonesho haya yameanza rasmi leo tarehe 05.12.2019 na kilele chake itakuwa ni tarehe 09.12.2019 Banda la Jatu ni namba 32 wote mnakaribishwa kujifunza fursa mbalimbali za Jatu na kujipatia bidhaa bora zinazoandaliwa na viwanda vya Jatu pamoja na huduma kuhusu Jatu Sacoss.

jatu yaanza utafiti kilimo cha matunda muheza, tanga

Kampuni ya JATU PLC kwa kushirikiana na wanachama wake wanazidi kusonga mbele kwenye uwekezaji wa sekta ya kilimo cha kisasa baada ya hivi punde kuanza rasmi utafiti kwenye kilimo cha matunda zao la mchungwa wilayani Muheza, Tanga. Hatua hii imefikiwa baada ya wiki chache zilizopita Mkurugenzi mtendaji wa JATU PLC Ndg. Peter Isare kualikwa kwenye ofisi za mkurugenzi wa halmashauri Muheza na kufanya kikao na viongozi wa wilaya na kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji ndani ya Muheza.

Timu yetu ya utafiti ikiongozwa na Mr. Paul Kapalata imeshapiga kambi wilayani Muheza na hadi sasa inaendelea na utafiti kwa kuangalia aina mbalimbali za mbegu na ubora wake, vipimo vya udongo, magonjwa, wadudu waharibifu na aina za mbolea n.k. Matokeo ya utafiti huu yatafungua ukarasa mpya kwa wakulima wa JATU ambao wamekua wakihitaji kuwekeza kwenye kilimo cha matunda kwa muda sasa.

ofisi ya kilimo, mifugo na uVUVI morogoro yafurahia semina za jatu

Wakazi wa Morogoro leo katika ofisi za idara ya kilimo, mifugo na uvuvi wamefurahishwa sana juu ya uwepo wa Jatu Plc kuwapatia semina. Hakika wamepata mwamko mkubwa wa kujiunga hususa kupitia huduma za Kilimo, Viwanda ,Masoko na Mikopo.
#JATU NI FURSA YA KILA MTANZANIA
#WEKEZA JATU LEO KWA FAIDA YA MAISHA YAKO.

Kwa maelezo zaidi:
📞0657 779 244

Au tembelea tovuti zetu:
🌎www.jatukilimo.com
🌎www.jatu.co.tz

mkurugenzi wa jatu akutana na viongozi wa halmashauri ya kondoa-DODOMA

Jumatatu tarehe 25.11.2019 Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya JATU PLC Ndg. Peter Isare akiwa katika mkoa wa Dodoma halmashauri ya wilaya ya Kondao na viongozi mbalimbali wa halmashauri akiwemo Mwenyekiti wa halmashauri ndugu. Hamza Mafita pamoja na kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya kondoa mjini ambaye pia ni Afisa kilimo wilaya ya kondoa.
Lengo ni majadiliano kuusu JATU PLC kuwekeza fursa mbalimbali kwa wakazi wa kondoa husasa katika fursa za Kilimo. Viongozi wa halmashauri hiyo Wamesema tayari wanalo eneo la takribani ekari 3,000 ambalo tayari lilishafanyiwa upepumbuzi yakinifu na Wako tayari kufanya kazi na Jatu Plc kwa nia ya kujenga Afya na kutokomeza umasikini kwa wakazi wa Kondoa.

#WEKEZA NA JATU LEO.

Kwa maelezo zaidi:
Simu: 0657 779 244

HALMASHAURI YA MUHEZA-TANGA YAahidi KUSHIRIKIANA NA JATU KUWEKEZA KWENYE KIWANDA CHA MATUNDA

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya JATU PLC Ndg. Peter Isare akiwa na viongozi mbalimbali katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya muheza ya mkoa wa Tanga, viongozi hao ni pamoja na Mbunge wa Muheza Mhe. Balozi Adadi Rajabu, Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe. Nassib Mmbaga na Mwenyeketi wa halmashauri ya Muheza Mhe.Bakari Mhando. Lengo la mazungumzo ni namna gani ambavyo JATU PLC inaweza kuwekeza katika kilimo cha matunda (machungwa) na kuanzisha kiwanda cha vinywaji hasa maji na juisi katika wilaya ya Muheza-Tanga ambapo Uongozi wa Muheza umesema uko tayari kutoa eneo la ujenzi wa kiwanda na eneo kwa ajili ya kilimo cha kisasa.

#WEKEZA JATU LEO UWE KATIKA MNYORORO WA THAMANI.

WAKAZI WA BUMBULI-TANGA WAFURAHIA UJIO WA SEMINA ZA JATU

Semina za JATU , Bumbuli Tanga🔥

Vijiji vifuatavyo vimeshiriki kijiji cha kwalei, kwadoe , kwakitui, soni, Baga, kwengala na Bumbuli. JATU imeahidi kushirikiana na wakazi hao ili kuwawezesha kulima kisasa bila stress na JATU, kuwawezesha kula kwa faida kupitia bidhaa za JATU na kushirikiana nao katika kupata soko la uhakika wa mazao ya kilimo na ufugaji yanayozalishwa na wakazi hao.

Wanabumbuli kwa ujumla wamefurahishwa sana na semina hizi.

Jenga Afya Tokomeza Umasikini.

TUPO TAYARI KUKUHUDUMIA FIKA OFISI ZETU ZILIZO KARIBU NAWE

Tumejipanga kuhakikisha unapata huduma bora wakati wote fika ofisi zetu zilizo karibu nawe tunapatikana mikoa ifuatayo;

  1. ARUSHA
  2. MWANZA
  3. MTWARA
  4. DAR ES SALAAM(SABASABA)
  5. DAR ES SALAAM(POSTA)
  6. DODOMA

KARIBU TULIME BILA STRESS MPUNGA NA MAHARAGE KWA AWAMU NYINGINE TENA

Kutokana na Uhitaji wa mashamba kwa wanachama wa kampuni ya JATU kuwa mkubwa. JATU PLC wamefungua tena nafasi ya kuomba mashamba na kushiriki katika mradi wa kilimo na kampuni ya JATU.

Kilimo cha maharage Kilindi, Tanga – Ekari 500 (Kukodi) @Tshs. 100,000/=

Kilimo cha mpunga Kilombero, Morogoro – Ekari 500 (Kukodi) @Tshs. 100,000/=.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KITETO YAAHIDI KUWAPATIA JATU PLC ENEO LA UJENZI WA KIWANDA CHA NYAMA

Kwenye uzinduzi wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha wanajatu Kiteto-Manyara ambapo viongozi mbalimbali wa serikali walihudhuria akiwepo na Mkurugenzi wa halmashauri ya Kiteto Bw. Tamimu Kambona(mwenye suti katikati) ambae amepongeza juhudi za JATU katika kuwaletea maendeleo wanakiteto na wanajatu kiujumla na wakazi wa kijiji cha matui ambapo ndo mradi huo unatekelezwa kwa kuisaidia serikali kutatua kero ya maji katika eneo hilo. Kwa kuunga mkono juhudi hizo ameahidi kutoa eneo kwa kampuni ya JATU ili iweze kujenga kiwanda cha nyama ili kusaidia upatikanaji wa soko la uhakika kwa wanakiteto ambao asilimia kubwa ni wafugaji na wakulima.

JATU PLC YAZINDUA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KITETO MANYARA

Ile ndoto ya wanajatu ya kufanya kilimo cha umwagiliaji imetimia baada ya kuzindua rasmi mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwenye shamba lililopo kijiji cha Matui, Kiteto Manyara. Hafla hiyo iliyohudhuria na wanakilimo wa JATU, wanakijiji wa matui, wadau wa maendeleo ya kilimo nchini, SAGCOT na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mr. Tamimu Kambona walifurahishwa na kuanzishwa kwa mradi huo kwani utakua mkombozi kwa wakulima wa Kiteto kwani wilaya hiyo inakabiliwa na ukame hivyo kilimo cha umwagiliaji ndo njia pekee ya kufanya mageuzi kwa maendeleo ya kilimo wilayani humo, ila pia ameipongeza JATU kwa kusaidia wanakijiji wa jirani na eneo la mradi kwa kuwapatia maji ya uhakika kwani wananchi wa maeneo hayo hawajawahi kuwa na maji safi. Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi wa JATU PLC Ndugu Peter Isare alisema, “Haikua rahisi kufika hapa leo mpaka tunazindua mradi wetu nawapongeza sana wakulima wa JATU, viongozi wa serikali, wanakijiji kwa kushirikiana nasi hadi leo tunafanya uzinduzi rasmi, tuwaahidi kuwa mradi huu utakua mkombozi sio tu kwa wakulima wetu bali hadi kwa wanakijiji wa Matui ambao ndo majirani zetu”

JATU PLC YAALIKWA BUNGENI DODOMA

Leo timu ya Jatu PLC ikiongozwa na Mkurugenzi wetu Ndg. Peter Isare imetembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tulipata wasaha wa kuwa na mkutano uliwahusisha Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu; Bunge, sera, ajira, kazi na wenye ulemavu, Mhe. JENNISTER MHAGAMA, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Katiba na sheria ambaye pia ndie Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mhe. Najima Giga. Pia mkutano huu ulihusisha Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge, Sheria na Katiba pamoja na viongozi wakuu wa idara ya vijana ofisi ya Waziri mkuu.

Kamati nzima imefurahishwa na ujumbe mzito kutoka Jatu na kuahidi kuendelea kushirikiana na kampuni yetu na pia kuhamasisha wabunge na mawaziri kuzitumia fursa za JATU hasa kipindi hiki tunapoelekea soko la hisa. Sisi kama JATU tunayo furaha kubwa kupata nafasi hii ya kipekee na kuwaahidi wanachama wetu kuwa tutaendelea kuipeleka JATU mbali zaidi na hatimae kutimiza malengo tuliyojiwekea. Tunaendelea kuwakaribisha wananchi wengine kuja kuwekeza JATU na kuzidi kuwapongeza wanachama wetu kwa kutuamini na kuwa nasi pamoja mpaka, JATU tunaamini penye nia pana njia ndio maana tulianza kwa kutambaa, tukasimama na sasa tunatembea tukibeba mafanikio kwa pamoja.

JATU PLC YATIMIZA MIAKA MITATU TANGU KUANZISHWA RASMI

Katika kuadhimisha miaka 3 ya JATU PLC,tumefanikiwa kupata wasaa wa kutembelea kituo cha wazee wasio jiweza na wenye ulemavu cha serikali kilichopo Kigamboni vijibweni eneo la Nunge kilichopo chini ya Wizara ya Afya Jamii jinsia wazee na watoto.

Tunapotimiza miaka mitatu ya kampuni yetu tunafurahia misingi ya umoja, bidii, ubunifu, uthubutu na huduma bora.” Endelea kufurahia kuwa mwanachama wetu.

JATU~Jenga Afya tokomeza umasikini.

SAFARI YA JATU PLC KUELEKEA SOKO LA HISA DSE YAZIDI KUPAMBA MOTO

Ikiwa imebaki muda mchache kuelekea soko la hisa Dar es salaam(DSE) kampuni ya JATU imewataka watu wote wanaohitaji kumiliki hisa za JATU baada ya soko kufunguliwa kuweka ahadi kwa kujaza fomu maalumu ikionesha taarifa zao na idadi ya hisa watazonunua. Kima cha chini cha kununua ni hisa 50 na kuendelea, kumbuka ili ushiriki kwenye fursa mbalimbali na JATU kama kilimo, Saccos, bima ya afya, mikopo isio na riba n.k ni kuwa sehemu ya umiliki wa kampuni ya JATU PLC. Ukishajaza utaituma kwenye barua pepe: ipo@jatu.co.tz au bonyeza link hapo chini kujaza fomu online

https://jatu.co.tz/admin/en/dse_registration

“Miliki hisa za JATU kwa faida ya maisha yako ya leo na kesho”

JATU INAKULETEA SAFARI YA KITETO

JATU PLC inawaletea safari ya Kiteto, ni safari maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya JATU PLC kwaajili ya wakulima na wanachama wa JATU ikishirikisha viongozi wa kiserikali na wadau wa maendeleo ya kilimo. Tutajifunza mengi kuhusu kilimo cha JATU cha umwagiliaji na mustakabali wa kilimo cha JATU kwa msimu wa mwaka 2019/20 kupitia mkutano wa wakulima utaofanyika hapo Kiteto. Tutaanza safari Ijumaa ya tarehe 15/11/2019 na kurudi Jumapili ya tarehe 17/11/2019, gharama za safari ni 100,000/= ambayo itahusu nauli, chakula siku ya tukio na Tshirt na kofia ya JATU. Yoyote anaruhusiwa kushiriki hata kama sio mwanachama malipo wasiliana nasi kupitia namba +255 657 779 244

“Twenzetu Kiteto tukajionee nchi yetu ya ahadi”

SASA UNAWEZA KUPIGA SIMU BURE JATU HUDUMA KWA WATEJA

JATU imerahisisha huduma ya mawasiliano, sasa unaweza kupiga simu BURE upate huduma kwa haraka na njia rahisi kabisa. Namba zetu za kupiga simu bure ni 0800 7500 97

MASHAMBA YA UMWAGILIAJI YA JATU KITETO SASA YANAPATIKANA, UNASUBIRI NINI?

Baada ya zaidi ya miaka mitatu kwenye kilimo wilayani Kiteto sasa tunazidi kusonga mbele kwa kasi na sasa JATU imeamua kutekeleza maazimio yake ya kuja na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa lengo la kuongeza tija kwa wakulima wetu ambao wamekua nasi bega kwa bega. Tulianza kwa kufanya utafiti wa kina wa kutafuta vyanzo vya maji, ambapo tulileta matumaini mapya kwa wakulima baada ya kupata uhakika wa chanzo cha maji yaani water table. Baada ya kukamilisha zoezi la utafiti tulianza uchimbaji maji kwa kutumia mitambo maalumu ya kisasa, zoezi hili limefanikiwa na sasa kilimo cha umwagiliaji cha JATU kitaanza kimeanza rasmi. Hivyo Kampuni ya JATU PLC inayofuraha kukutangazia wewe mtanzania uliyekosa nafasi ya kumiliki shamba la umwagiliaji katika msimu uliopita, sasa yanapatikana kwa gharama ya shilingi laki saba na nusu kwa hekari moja ambapo mpaka sasa zipo hekari 500. Mashamba ya umwagiliaji yanapatikana kupitia APP ya JATU iliyopo play store. Kuanza rasmi kwa mradi huu ni fahari kubwa kwa wakulima wa JATU na watanzania wengine ambao wangependa kushiriki kwenye miradi ya kilimo na JATU, kwa pamoja tunasema “Kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji kinawezekana”.

BREAKING NEWS: TONE LA KWANZA LIMERUKA… KITETO YAGEUKA KUWA NCHI YA ASALI NA MAZIWA

Kiteto ni wilaya yenye ardhi yenye rutuba nyingi kwaajili ya kilimo japokua inakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji kutokana na asili ya eneo hilo kuwa nusu jangwa. JATU kwa kushirikiana na wanachama wake waliiona fursa ya uwekezaji nakuamua kuanzisha mradi wa kilimo cha Alizeti na mahindi, kilimo hiki kilitegemea mvua za msimu kwa miaka zaidi ya miwili tukikabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa, kitu ambacho kilisababisha mavuno kutokua lukuki. Tunazidi kusonga mbele kwa kasi na sasa JATU imeamua kutekeleza maazimio yake ya kuja na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa lengo la kuongeza tija kwa wakulima wetu ambao wamekua nasi bega kwa bega. Tulianza kwa kufanya utafiti wa kina wa kutafuta vyanzo vya maji, ambapo tulileta matumaini mapya kwa wakulima baada ya kupata uhakika wa chanzo cha maji yaani water table.

JATU YAALIKWA KWENYE MKUTANO WA WAWEKEZAJI WA MAZAO YA NAFAKA

Jatu Plc imepata nafasi ya kualikwa na Wizara ya Kilimo katika mkutano wa siku mbili (29.08.2019 – 30.08.2019), Mkutano huo unawakutanisha wafanyabiashara na wadau wa nafaka nchini pamoja na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na kujadili fursa mbalimbali zilizopo katika tasnia hiyo ya nafaka na jinsi ya kuzitumia ikiwa ni pamoja na Masoko. Jatu katika mkutano huo inawakirishwa vyema na Eng. Dr. Zaipuna Obedi Yonah ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi Jatu Plc. Jatu inatoa shukrani kwa Wizara ya Kilimo kwa mualiko huo, na kuwaahidi wanachama wetu kuwa, tutaitumia fursa hii vyema katika kutanua wigo wa biashara yetu ya mazao ya nafaka na Masoko kwa ujumla ili kufikia lengo letu la kujenga Afya na kutokomeza umaskini kupitia Kilimo, Viwanda na Masoko.

MRADI WA KILIMO CHA JATU CHA UMWAGILIAJI KITETO WAANZA RASMI

Mkurugenzi wa Kampuni ya JATU PLC, Ndugu Peter Isare amethibitisha maandalizi ya kufunga mitambo na kuchimba visima kwaajili ya mradi wa umwagiliaji kwenye mashamba ya Kiteto, Manyara yameanza rasmi. Malengo ya kampuni ni mpaka ifikapo mwakani asilimia kubwa ya shamba iwe tayari kwenye umwagiliaji hii itaongeza thamani ya uwekezaji kwenye mradi huu na kufanya wakulima wetu kulima pasipo kutegemea msimu wala mvua. JATU imejidhatiti kwenye kuboresha maisha ya watanzania kupitia uwekezaji kwenye kilimo na viwanda hivyo inaendelea kuwashauri wadau wenye ndoto ya kuwekeza kwenye kilimo kuitumia hii fursa adhimu ya kilimo cha JATU ambacho hakikusumbui kwenye usimamizi, utapatiwa mkopo usio na riba na chenye uhakika wa soko kufanikisha ndoto zao.

KULA ULIPWE NA JATU PLC

Je wajua ukinunua bidhaa za JATU PLC unalipwa? Hakika ukiweka oda yako ya bidhaa za JATU kupitia kwenye APP ya JATU utaweza kula kwa faida ambapo utalipwa kwa kila manunuzi yako na ya wanamtandao wako. Pia ukiweka oda yenye thamani ya kuanzia 30,000/= utaletewa mpaka ulipo bure kabisa. Weka oda ya Mchele, Unga wa sembe na dona, mafuta ya alizeti, maharage na karanga sasa.

JATU YATANGAZA NEEMA KWA WAKULIMA WA MAHARAGE KILINDI

JATU PLC inawatangazia wana kilimo cha maharage mradi unaofanyika Kilindi, Tanga na kuwa zoezi la mavuno ya limekamilika, hivyo wanashauriwa kufuatilia mtiririko wa bei za zao hilo ili waweze kuuza mazao yao kupitia kampuni ya JATU PLC. Unaweza kupiga simu kwa mkuu wetu wa Idara ya Fedha kupitia namba 0657 093807 uweze kuhudumiwa

POSTA TUMEWAFIKIA TUPO PPF HOUSE

Kampuni ya JATU PLC ili kusogeza huduma karibu zaidi kwa wateja wake wa Dar es salaam imefungua ofisi maalumu kwaajili ya idara ya masoko ambayo inapatikana Posta mtaa wa Samora jengo la PPF House ghorofa ya 6. Ofisi hii inaendesha semina kwa wanachama, wadau na mabalozi wa JATU kila Jumamosi ukumbi uliopo ghorofa ya 11 hapo hapo PPF House. Nyote mnakaribishwa

Fursa kwa wafanyabiashara wa mchele

JATU PLC inawatangazia wafanyabiashara wote wa mchele kuwa tunapokea oda za kununua mchele wa JATU ambao ni mchele super kabisa na hauna chenga. Unaweza kaugiza kiasi chochote unachoweza kwa kutupigia simu 0768 342 943. Ukiagiza kuanzia tani 1 utaletewa mpaka ulipo, tuna Grade A, B na C kwa bei nafuu. Pia mnaweza fika kwenye ofisi zetu zilizopo Sabasaba, Dar es Salaam kwa maelezo zaidi.

JATU yatangaza neema kwa wakulima wa Mpunga, Morogoro

Kampuni ya JATU PLC imetangaza neema kwa wakulima wa JATU walioshiriki kwenye kilimo cha mpunga wilayani Kilombero, Morogoro baada ya timu ya kilimo ya JATU kutembelea mashamba hayo ambayo mazao yake yamekomaa hivyo kuwa tayari kwa uvunaji. JATU imetangaza kuwa kuanzia tarehe 17/06/2019 mavuno yataanza hivyo wakulima wanaweza kufika au kutuma mwakilishi kwenye ofisi yetu ya Mbingu pale kwenye kiwanda chetu cha mpunga kushuhudia zoezi zima la uvunaji. Baada ya hili zoezi kukamilika kutakua na kikao cha wanakilimo kufanya tathmini ya huu mradi kiujumla.

Msimu wa Kilimo cha Mahindi na JATU umewadia

JATU PLC inawajulisha wanahisa na wadau wa kilimo kuwa msimu mpya wa kilimo cha mahindi umeanza hivyo tumeanza kupokea maombi ya ushiriki. Mradi huo unaofanyika tangu mwaka 2016 wilayani Kiteto, Manyara na ambao umekua na matokeo chanya tangu uanzishwe na kuwakomboa wakulima wengi umeanza tena. Jiunge nasi upate mkopo usio na riba kwa kilimo

JATU yazidi kung’ara kwenye kilimo cha Alizeti – Kiteto, Manyara

JATU PLC imetangaza neema kwa wakulima wake walioshiriki mradi wa kilimo cha Alizeti Wilayani Kiteto, Manyara na kuwaambia wajipange kwa mavuno mazuri baada ya Mkurugenzi Peter Isare kujihakikishia hilo alipotembelea mashamba hayo hapo jana. Mkurugenzi wa JATU Peter Isare alisema, “Hii ni faraja kubwa sana kwa wakulima wa JATU kwani mazao yao yamenawiri sana na hii inaonesha ni jinsi gani Mungu yupo pamoja nasisi”.

JATU imetoa matumaini mapya kwa wakulima wa maharage

Kampuni ya JATU PLC imezidi kutoa neema wa wakulima wake wa maharage hasa juu ya mradi wake wa kilimo cha maharage unaofanyika Kilindi, Tanga ambapo zaidi ya ekari 200 zimelimwa na zinategemewa kutoa mavuno mazuri kwa hiyo kutoa tumaini jipya kwa wakulima hao ambao wamekua wakisuasua kabla ya JATU kuamua kushiriki nao ili kuleta tija kwenye zao hilo.

HISA za JATU zimefikia patamu

Kampuni ya JATU imezidi kuliteka soko la hisa baada ya kutangaza hatua yake ya kwenda IPO kupitia soko la DSE. Hatua hii imepongezwa na Mkuu wa Wilaya wa Temeke Mh. Felix Lyaniva alipohudhuria mkutano wa wanahisa wa JATU na wadau wa maendeleo uliofanyika Jumamosi ya tarehe 1/6/2019 pale Isamuhuyo Hall JKT Mgulani. Mh Felix alisema, “Sasa naiona JATU ikizidi kupaa juu zaidi hakika ni vijana wa mfano wa kuigwa hili suala sio rahisi lakini wameweza, najivunia kuwa na vijana hawa ndani ya wilaya yangu ya Temeke”

Serikali imeipongeza bodi mpya ya JATU PLC

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Afisa Maendeleo ya Vijana Mwandamizi) Ndugu ELIAKIM E. MTAWA aliehudhuria mkutano wa JATU uliofanyika hivi karibuni alisema bodi mpya inafanya kazi kwa bidii na imebeba maono ya wanahisa hivyo ameitaka kusimamia misingi ya wanahisa ili kuhakikisha JATU inasonga mbele na serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha lengo la JATU la kuwakomboa wakulima linatimia.

JATU PLC yaamua kubadili gia na kuja na kilimo cha kisasa zaidi

Kampuni ya JATU PLC imebainisha baadhi ya mipango yake kwenye sekta ya kilimo na viwanda kwa kuja na mpango kazi wa kuhakikisha unawekeza kwenye miradi ya umwagiliaji ya kisasa kwenye mashamba yake yote. Hii imebainishwa na mjumbe wa bodi ya JATU PLC Mhandisi Ian Samakande ambae ni mtaalamu wa kilimo cha Umwagiliaji alipokua akijibu swali la mwanachama wa JATU PLC kwenye mkutano uliofanyika hivi karibuni.

Tutembelee kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii

OUR PARTNERS

Tutumie Ujumbe


Copyright JATU Public Limited Company 2019 – All rights reserved